0




Timu ya maafande wa Polisi Mara mara kesho watapigishana kwata na maafande wenzao wa Polisi Tabora katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza utakaofanyika katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjni Tabora.

Akizungumza na Blog hii,Mwenyekiti wa timu ya Polisi Mara Alon Mihayo amesema kikosi cha timu hiyo kimefika salama mjni Tabora na wapo tayari kushuka dimbani hapo kesho kuvaana na maafande wenzao wa Tabora.

Amesema kuwa mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na kila timu kuhitaji ushindi katika mchezo huo ili kujiweka katikia mazingira mazuri katika msimamo wa kundi hilo linaloongozwa na timu ya maafande wa JKT Kanembwa ya Kigoma yenye pointi 23 ikifuatiwa na wanajeshi wa Rhino ya Tabora yenye pointi 19.

Katika kundi hilo timu ya Polisi Mara inashika nafasi ya 5 kati ya timu saba ikiwa na pointi 10 hivyo mchezo huo una umuhimu kwao katika kuijiweka katika mazingira mazuri.

Post a Comment