0




Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa maarum wa kipolisi Tarime/Rorya Justus Kamugisha amesema baada ya timu ya soka ya Polisi Tarime kufanikiwa kuingia hatua ya fainali ya ligi ya mkoa wa Mara ofisi yake kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watahakikisha timu hiyo inafanya vizuri na hatimaye kuchukua ubingwa wa mkoa wa Mara.

Akizungumza na Blog hii,Kamugisha amesema kuwa amefarijika sana na timu hiyo kuingia katika hatua hiyo na atjitahidi kwa kushirikiana na wadau kuhakikisha malengo ya kupanda daraja kwa timu hiyo yanafanikiwa.

Amesema siri ya ushindi wa timu hiyo ni kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya kwa muda mrefu ikiwa chini ya mwalimu Augustine ambaye amekitengeneza kikosi cha timu hiyo ambacho kwa sasa matunda yake yanaonekana.

Kamugisha amesema timu hiyo sio ya Jeshi la polisi peke yake bali ni timu ya Wananchi wote wa Wilaya ya Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla hivyo kila mmoja anapaswa kuiunga mkono timu hiyo.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa timu hiyo Feluz Ahmed amesema ili kufanya vizuri katika hatua hiyo kunahitajika ushirikiano wa kila mmoja kwa kuwa hatua ya fainali ya nne bora kila timu imejipanga kuhakikisha wanakuwa mabingwa wa mkoa kwa msimu huu.

Feluz amesema kwa kuanzia wadau wote wanatakiwa kuweka nguvu zao katika mchezo wao wa kwanza hapo kesho dhidi ya Bunda Town Star mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa sabasaba mjini Bunda. 

Timu nyingine ambazo zimefanikiwa kuingia katika hatua hiyo ya nne bora katika kutafuta bingwa wa soka mkoa wa Mara kwa msimu huu ni pamoja na Polisi Bunda,Musoma Shooting,Polisi Tarime pamoja na Bunda Town Stars.

Post a Comment