Siku nne baada ya kupiga kura wakenya wangali kujua
mshindi, wa urais, baadhi ya yaliyojitokeza hadi sasa ni pamoja na
malalamishi ya muungano wa CORD wake Raila Odinga kutaka tume ya
uchaguzi kusitisha shughuli ya kuhesabu kura wakidai kufanyika
udanganyifu.
Leo mashirika ya kijamii yamekwenda mahakamani kuitaka mahakama kuu kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura
Hadi kufikia sasa Uhuru Kenyatta ana kura 5,004,406 Raila Odinga ana kura 4,442,923
Wakenya wakiwa katika kipindi kigumu na cha wasiwasi kwani imechukua Tume ya Uchaguzi muda wa siku nne tangu kuanza shughuli ya kuhesabu kura na bado mshindi hajajulikana.
Kumekuwa na kila aina ya matukio katika muda huo wote. Tayari mashirika ya kijamii yameitaka mahakama kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura inayofanywa na tume ya uchaguzi.
Muungano wa CORD unaoongozwa na tume ya uchaguzi, umelalamika ukisema shughuli hiyo ina mizengwe na wanataka ianzishwe upya.
Post a Comment
0 comments