Kivumbi cha
mashindano ya Ester cup kwa mwaka wa tatu mfulululizo kimeanza kutimua vumbi
katika uwanja wa sabasaba mjini hapa huku jumla timu 38 zikijitokeza kuwania
kitita cha shilingi milioni moja.
Akifungua mashindano
hayo ambayo kwa msimu huu yamekuwa na hamasa kubwa kutokana na kuongezwa kwa
zawadi na timu zinazoshiriki,afisa michezo wa Wilaya ya Bunda Amosi Mtani
alisema mashindano hayo yamekuwa na mafanikio makubwa tangu yalipoanzishwa
mwaka 2011.
Alisema kupitia
mashindano hayo kiwango cha soka katika Wilaya ya Bunda kimepanda na vipaji
vingi vimeonekana kupitia michezo hiyo ikiwemo timu nyingi kujisajili kupitia
ofisi ya michezo na utamaduni na hivyo kuongeza ushindani wa timu.
"Leo ni mwaka wa
tatu mashindano haya yanafanyika na kila mmoja anaona mafanikio ambayo
yameonekana kupitia mashindano haya ikiwemo wachezaji wengi walioipa ubingwa wa
mkoa timu ya Polisi Bunda msimu huu wametokea katika mashindano haya.
"Kila mwaka
bingwa wa soka mkoa wa Mara amekuwa akitoka Musoma lakini kwa msimu huu kwa
zaidi ya miaka 15 tumeshuhudia bingwa akitoka katika Wilaya ya Bunda na bila
kuuma maneno nikiwa kama afisa michezo wa Wilaya hii nampongeza sana Mbunge
Bulaya kwa jitihada zake za kuibua vipaji na kuendeleza soka katika Wilaya
hii,"alisema Mtani.
Afisa huyo aliwataka
vijana kuyatumia mashindano hayo kuonyesha vipaji vyao nakucheza kwa malengo ya
kufika mabli kutokea katika mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mwaka wa
tatu mfululizo.
Katika michezo wa
kwanza wa ufunguzi,timu ya Majengo fc iliisambaratisha timu ya Bunda yosso
Academy kwa kuifunga mabao 4-2 kabla ya mchezo wa pili timu ya Guta fc
kuibamiza timu ya panda miti mabao 3-0.
Bingwa mashindano
hayo kwa mwaka huu ataondoka na kitita cha shilingi milioni moja pamoja na
kombe,mshindi wa pili laki tano,mshindi wa tatu laki tatu,timu yenye nidhamu
lakini moja huku mchezaji bora na mfungaji bora kila mmoja akichomoza na
shilingi elfu hamsini.
Post a Comment
0 comments