MBUNGE
wa viti maalumu mkoani Mara kupitia vijana Ester Bulaya (CCM)
amewahimiza waimbaji na watunzi wa nyimbo kutunga nyimbo za kuhimiza
amani katika Taifa kutokana na
kuibuka kwa matukio ambayo yanaweza kuatalisha amani na kupelekea
kutokea kwa vurugu.
Kauli hiyo aliitoa juzi Mjini Bunda alipokuwa akizindua kikundi cha
uimbaji wa nyimbo za Injili cha Disciples of Crist Bunda pamoja na
kutambulisha album yao ya kwanza, ambacho licha ya kujishughulisha na
uimbaji kinafanya kazi za utetezi wa haki za binadamu na utunzaji wa
mazingira.
Alisema
katika siku za hivi karibuni kumeibuka matukio ambayo yanaweza
kuhatalisha amani iwapomakundi mbalimbali katika jamii hayatachukua
hatua za kuelimisha namna ambavyo hatari kubwa inaweza ikatokea kutokana
nakukosekana kwa amnai.
Bulaya
alisema amani ni kitu muhimu muhimu katika Taifa ambapo inapokosekana
inamuathiri kila mmoja hivyo hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa
ilikuweza kuondosha hali yoyote ambayo kwa namna moja inaweza
kuhatalisha amani.
Alisema
kwa sasa watu wengi katika jamii wamekuwa wakisikiliza nyimbo
mbalimbali hususani za injili hivyo waimbaji na watunzi wanaweza
kuitumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kupitia nyimbo hizo za injili ili
hali hiyo isiweze kutokea katika Taifa.
"Kwanza
niwashukuru kikundi cha Disciples kwa kazi kubwa mlioifanya na hii leo
mnazindua kikundi chenu pamoja na album yenu ya kwanza kama wana
kikundi,nyie ni watu muhimu ambao mnaweza kusisitaza amani kupitia
nyimbo zenu,nawaomba mtunge nyimbo za kusisitiza jambo hilo.
"Amani
inapokosekana katika Taifa ni janga ambalo litamgusa kila mmoja bila
kujali nafasi yake wala kazi hivyo lazima kupitia nyimbo jamii ijue
madhara ya kutokuwa na amani katika Taifa ambayo ikikosekana hakuna
lolote litakalo fanyika,"alisema Bulaya.
Mbunge
huyo alisema amefurahishwa na kazi zinazofanywa ka kikundi hicho ambapo
licha uimbaji amedai kazi za utunzaji wa mazingira na utetezi wa haki
za binadamu ni kitu muhimu katika jamii na kuahidi kukisaidia kikundi
hicho katika malengo yake waliyojiwekea.
Alisema
kikundi hicho kwa kuwa kimesajiliwa kinayo nafasi ya kupata mikopo ya
kuendeleza shughuli zao kwa kuwa katika mwaka huu wa fedha Serikali
imetenga kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya vijana.
Album ya kwanza ya kikundi hicho kilichozinduliwa imebeba nyimbo za Mateso,Laiti Tungelijua,Amri ya Mungu,Moyo wa Subira,Yesu
Anaweza,Yesu Mokozi,Huyu ndio Yesu na Yu Mwema ambayo tayari imeshasambazwa katika maeneo mbalimbali.
Post a Comment
0 comments