KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani
Bunda maarufu kama Kamanda Pius amesema lengo lake ni kuhakikisha vipaji vya
vijana katika Wilaya hiyo vinainuka na kuwa ni moja ya njia za kuongeza ajira
kupitia michezo.
Pius alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita alipokuwa
akikabidhi zawadi mbalimbali za vikombe mipira,jezi pamoja na fedha taslim kwa
mashindi wa mashindano ya Pius Cup yaliyomalizika wilayani Bunda katika uwanja
wa sabasaba.
Amesema ataendelea kuboresha mashindano na kuongeza zawadi
katika mashindano hayo ambayo amepanga kuyafanya kila mwaka ili kuongeza chachu
ya na kuwafanya vijana wengi kujitokeza
kushiriki.
Katika fainali ya mashindano hayo timu ya Amani fc iliibuka
mabingwa kwa kuifunga Kiwasi fc kwa changamoto ya penati 5-4 baada ya kumalika
dakika 120 bila timu hizo kufungana.
Kwa kuibuka mabingwa,timu ya amani ilikabidhiwa kikombe
kikubwa,medali pamoja na fedha taslimu shilingi laki sita huku washindi wa pili
wakichomoza na laki nne pamoja na kikombe.
Zawadi nyngine zilikwenda kwa mshindi wa nne shilingi elfu
hamsini,mshindi wa tatu laki mbili,timu bora ilichukua kikombe pamoja na
mpira,mchezaji bora,kipa bora,mfungaji bora pamoja na timu yenye nidhamu kila
mmoja alipata kikombe,medali pamoja fedha taslim shilingi elfu ishirini
|
Post a Comment
0 comments