WAZAZI na
Walezi wametakiwa kuzingatia malezi bora kwa vijana ili wasije kujiingiza
katika matumizi ya dawa za kulenya kwa kuiga tabia za makundi hatarishi na
kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Kauli hiyo
ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rorya Samwer Kiboye
katika mahafari ya tano ya dalasa la saba ya shule ya msingi Emanuel iliyopo
Manispaa ya Musoma.
Alisema
kutokana na wimbi la kuzuka kwa kasi kwa matumizi ya dawa za kulevya ni wajibu
wazazi na walezi pindi wanafunzi wanapohitimu elimu ya msingi na kuwa nyumbani
kuwalea katika malezi bora ili wasijiingize katika makundi hatarishi.
Kiboye
alisema katika kipindi hicho ni vyema wanafunzi kuwapa masomo ya ziada kuliko
kuwa mitaani hali ambayo inaweza kuwafanya kuingia kwenye makundi ya vijana ambao bado hawajabadilika na kushiriki vitendo
vibaya.
Alisema kwa
sasa Taifa limekuwa kwenye mjadala na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya na
athari ya matumizi yake hivyo kila mmoja anapaswa kuchukua hatua kupingana nayo.
Alisisitiza
kuwa madawa ya kulevya sio cocaine na mengineyo bali hata bangi ni dawa za
kulevya na ndio vijana wengi wamejiingiza katika matumizi yake na kuharibikiwa.
Aidha
Mwenyekiti huyo CCM Wilaya ya Rorya aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mahafari hayo
ya shule ya msingi Emanuel aliwataka wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi
katika shule hiyo kuwa watulivu katika chumba cha mtihani ili waweze kufanya
vizuri na hatimaye kujiunga na elimu ya sekondari hapo mwakani.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa shule hiyo Ester Marwa alisema hazina kubwa ambayo
anastahili mtoto kwa sasa ni elimu hivyo kuwaomba wazazi kuhakikisha vijana
wanakuwa na elimu bora kuanzia msingi,sekondari hadi vyuoni.
Post a Comment
0 comments