MAKAVERI MWENYE MIWANI NA MASHABIKI WA CARGO KABLA YA MCHEZO
MABINGWA CARGO FC WAZE WA KIZIGO
FEAR JAMANI
REFA DODOMA AKIPIGA KURA KUANZA MCHEZO
MAWINGA NA MAFUNDI WA MODER KUTOKA NYASHO MITUMBANI NAO WALIKUWEPO
NAHODHA FULUME AKITAMBULISHA
TUMEFUNGWA LAKINI POA
CHIKAKA NA LIMA NAO WALIKUWEPO
SEHEMU YA MASHABIKI
MRATIBU AMNAI RICHARD AKIELEZEA MASHINDANO HAYO
DC MSOME AKITOA NENO
ZAWADI YA MFUNGAJI BORA HIYO
MCHEZA BORA WA MASHNDANO AKIPOKEA ZAWADI YA JEZI KUTOA DUKA LA VIFAA VYA MICHEZO LA AMANI
NI KAMA ANAAMBIWA NA MKUU WA WILAYA,TENGENEZENI NIDHAMU KWENYE TIMU
NAHODHA WA CARGO FC FRUMENCE TUNGARAZA AKIPOKEA MPUNGA
NI KAMA VILE UNAWEZA KUSEMA TIMU NGENI KATIKA MASHINDANO YA
CARGO FC KUTOKA MAENEO YA MWIGOBERO NI KAMA INAZIMA ZAMA ZA KUTAMBA KWA TIMU
KONGWE YA KIGERA FC PALE ILIPOICHAPA TIMU YA KIGERA FC MABAO 2-1 KATIKA FAINALI
ZA MASHINDANO YA PETROLUX CUP YALIYOKUWA YAKIFANYIKA MANISPAA YA MUSOMA.
HII INAKUWA FANALI YA PILI KWA KIGERA FC KUPOTEZA KWA MWAKA
HUU BAADA YA KUFUNGWA AWALI KATIKA MASHINDANO YA BINDA CUP NA TIMU YA BEACH
BOYS KWA MIKWAJU YA PENATI 6-5 NA KUIFANYA TIMU HIYO IKITAFAKARI.
CARGO FC INAYONOLEWA NA KOCHA SINDBAD MADENGE AMBAYE PIA NI
MKUFUNZI WA MAKOCHA MKOANI MARA ILICHOMOZA NA KITITA CHA SHILINGI LAKI TANO
BAADA YA KUCHUKUA UBINGWA HUO HUKU KIGERA WAKIJIPOZA NA SHILINGI LAKI TATU.
KOCHA MADENGE BAADA YA KUCHUKUA UBINGWA HUO NA ULE
ALIOCHUKUA AWALI WA MASHINDANO YA DUME CONDOM SASA AMESEMA KILICHOBAKI NI TIMU
HIYO KUINGIZA KWENYE LIGI MSIMU HUU KWANI TAYARI IMESHA KOMAA.
MRATIBU WA MASHINDANO HAYO AMANI RICHARD JOSIA AMESEMA
MASHINDANO HAYO YALIKWENDA VIZURI LICHA YA KUWEPO KWA CHANGAMOTO NDOGO NA KUDAI
KUZIFANYIA KAZI KABLA YA MASHINDANO MENGINE.
AKIKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI MKUU WA WILAYA YA MUSOMA
JACKSON MSOME ALIZITAKA TIMU ZOTE KUENDELEA NA KUFANYA MAZOEZI KWANI UTARATIBU
WA KUFANYA MASHINDANO KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU MBAALIMBALI UTAKUWA UKIFANYIKA
MARA KWA MARA.
Post a Comment
0 comments