TAASISI ya mfuko wa uwekezaji kiuchumi katika tarafa ya Nyanja(NEIT) Halimashauri ya Musoma mkoani Mara inatarajia kuwekeza zaidi ya sh bilioni 52 katika sekta mbalimbali kwenye Kata 17 za wilaya hiyo ikiwa ni mkakati wa kupunguza umaskini unaowakabili wananchi.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya
(NEIT) Machumu alisema kwamba utekelezaji wa mkakati huo unatarajiwa
kuzinduliwa rasmi mwezi January mwakani ambapo hadi hivi sasa vikundi 63 vya
ujasiliamali na maendeleo vimekwisajiliwa katika taaasisi kama
wanachama na kufungua akaunti zao benki.
Machumu
alisema NEIT
itasaidia kupunguza umasikini wa Wananchi wa Kata 17 za Wilaya ya Musoma
katika sekta za Kilimo,Uvuvi,Ufugaji,Mazingira,Elimu na Afya ambapo
miradi mikubwa kupitia sekta hizo itatekelezwa katika kipindi cha miaka
mitano
ya mradi unaoanza mwaka huu wa fedha wa 2013/14.
Alisema lengo la uwekezaji huo ni
kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa Wananchi walio wengi vijijini wanaoabiliwa na
umaskini mkubwa ambapo baadhi ya miradi mikubwa iliyolengwa kutekelezwa katika
mkakati huo ni mapinduzi ya kijani katika sekta ya kilimo kwa kushirikiana na Serikali katika mpango wake wa Kilimo kwanza
kupitia ASDP na DADIPS.
Aliitaja miradi mingine
itakayotekelezwa ni pamoja na uanzishwaji wa benki kata (SACCOS), benki ya
Exim ambayo tayari imeshaonesha nia ya kujenga tawi katika Wilaya hiyo,boti za
uvuvi za kisasa,ujenzi wa chuo cha mafunzo ya kilimo,chuo cha uuguzi na afya
sanjari na ujenzi wa vituo 3 vya afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Askofu Alpha Modekaye Mashauri
aliwataka Wananchi wa Wilaya hiyo kuanzisha kilimo cha kufa na kupona ili
kuondokana na aibu ya kutegemea msaada wa chakula cha njaa toka serikalini kila
mara kwa kuwa na chakula cha kutosha katika kaya zao.
Askofu Mashauri alisema licha ya Halmashauri hiyo kuongoza kila mwaka kwa baa la njaa kati ya halmashauri sita
za mkoa wa Mara, nafasi bado ipo ya kuondokana na tatizo hilo kwa kufuata
kanuni bora za kilimo,kuachana na uvivu wa kutofanya kazi sanjari na kutumia
mbolea ya kupandia na kukuzia ya minjingu mazao.
Post a Comment
0 comments