KIKAO CHA BODI YA BARABARA
MENEJA WA TANROADS MKOA WA MARA EMANUEL KOROSO AKIZUNGUMZIA HALI YA BARABARA
KOROSO
MWENYEKITI WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MARA AMBAYE NI MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIONGOZA KIKAO
MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA MJINI VICENTI NYERERE KATIKATI NAE ALIKUWEPO
MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKOANO AKICHANGIA MASUALA YA BARABARA
MAADHI YA MAKANDARASI WA TANROADS WAKIFATILIA KIKAO HICHO KWA MAKINI
MKUU WA UHAMIAJI PIA ALIKUWEPO
MENEJA WA TANROADS MKOA WA MARA EMANUEL KOROSO AKIZUNGUMZIA HALI YA BARABARA
KOROSO
MWENYEKITI WA KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MARA AMBAYE NI MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIONGOZA KIKAO
MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA MJINI VICENTI NYERERE KATIKATI NAE ALIKUWEPO
MBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKOANO AKICHANGIA MASUALA YA BARABARA
MAADHI YA MAKANDARASI WA TANROADS WAKIFATILIA KIKAO HICHO KWA MAKINI
MKUU WA UHAMIAJI PIA ALIKUWEPO
SERIKALI imetenga jumla ya shilingi bilioni 12.7
bajeti ya matengenezo mbalimbali ya barabara na madaraja mkoani Mara kwa mwaka
wa fedha 2013/2014 ambapo jumla ya kilomita 1552.18 za barabara na madaraja 60 yalifanyiwa ukarabati
kuanzia septemba hadi desemba mwaka jana.
Hayo yameelezwa jana na meneja wakala wa barabara
TANROADS mkoani hapa Eng. Emmanuel Korroso wakati anawasilisha taarifa ya
utekelezaji na mapendekezo ya bajeti,matengenezo sambamba na miradi ya
maendeleo kwenye kikao cha wajumbe wa bodi ya barabara kilichofanyika ukumbi wa
uwekezaji ofisiya mkuu wa mkoa huo.
Alisema serikali pia imetenga shilingi 2,144.87 bilioni kwa ajili ya miradi
ya maendeleo kwenye barabara mbalimbali na kwamba kilomita 2.2 zitajengwa kwa
kiwango cha lami huku kilomita 45.5 zitakarabatiwa kwa changarawe katika wilaya
mbalimbali za mkoa huo.
‘’Jumla ya fedha iliyopangwa kwa mwaka wa fedha
2013/2014 ni shilingi 14.9 milioni kwa ajili ya kazi ya matengenezo na kazi za
miradi ya maendeleo ambapo fedha hizi ni ongezeko la asilimia 4 ikilinganishwa
na bajeti ya mwaka 2012/2013’’alisema Korroso na kuongeza.
‘’hadi
kufikia mwisho wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2013/2014 utekelezaji wa kazi
za matengenezo ulikuwa umefikia asilimia 66.’’
Akizungumzia miradi ya maendeleo inayotekelezwa
kitaifa meneja huyo wa wakala wa barabara mkoani humo alisema kuwa serikali
imetumia bilioni 85.363 kwenye ujenzi wa barabara kuu itokayo mkoani Simiyu
hadi manispaa ya wilaya ya Musoma mjini mkoani hapa.
Kilomita 74 kati ya kilomita 85.5 zimekamilika
ukarabati huu pia unahusisha ujenzi wa madaraja mawili makubwa ya Rubana na
Suguti ambayo tayari yamekamilika’’ aliongeza.
Hata hivyo alisema mradi huo unatekelezwa na
kampuni ya kichina ya M/s Chiko chini ya mhandisi mshauri wa mradi huo ambao ni Consulting Engineering Services (India) Private ltd ikishirikiana naNorplan(T)
ltd kampuni ya kizalendo.
Post a Comment
0 comments