Huku Ligi ya kandanda nchini Tanzania ikitarajia
kuanza mzunguko wake wa Pili Mwishoni mwa juma hili, Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) limesimamisha usajili wa mshambuliaji Emmanuel
Okwi kutoka Uganda katika timu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi
kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Katika FIFA kuna kesi tatu kuhusiana na suala la mchezaji huyo. Wakati Okwi ameishitaki klabu hiyo FIFA kwa kutomlipa mshahara, Etoile du Sahel imemshitaki mchezaji huyo kwa utoro. Nayo Simba imeishitaki Etoile du Sahel kwa kushindwa kuilipa ada ya mauzo ya mchezaji huyo ambayo ni dola za Marekani 300,000.
Hivyo, TFF imeiandikia FIFA kutaka kujua iwapo mchezaji huyo anaweza kucheza Ligi nchini Tanzania wakati Etoile du Sahel ikiwa imefungua kesi katika shirikisho hilo la kimataifa ikidai Okwi bado ni mchezaji wake.
Emmanuel Okwi ambaye aliwahi Kuichezea Simba kabla ya kuuzwa kwenye Klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia,alikaribishwa kwa mbwembwe na hoi hoi nyingi wakati alipokuja kuanza kuichezea Yanga mwishoni mwa mwaka uliopita ambapo katika mechi dhidi ya Simba alifunga bao 1 la kufutia machozi WAKATI Yanga ilipobamizwa bao 3-1 na Simba katika Mechi maalum kati ya watani hao wa jadi katika Soka la Tanzania.
Post a Comment
0 comments