0


Manchester United, kwa mara nyingine tena ilikiona cha mtema kuni pale ilipobanduliwa nje ya kinyanganyiro cha kuwania kombe la Ligi maarufu kama Capital one na timu inayoshikilia nafasi ya pili kutoka mkia kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier, Sunderland.

United ililazimika kuyaaga mashindano hayo baada ya kushindwa kupitia mikwaju ya penalti na Sunderland.

Baada ya muda wa kawaidia United ilikuwa ikiongoza kwa goli moja kwa bila, lakini kuwa walipoteza mechi ya awamu ya kwanza kwa magoli mawili kwa moja, mechi hiyo ilibidi kuongezwa dakika thelathini zaidi za ziada.

Katika muda huo wa ziada Sunderland nusura ifuzu moja kwa moja lakini sherehe hizo zilikatizwa baada ya dakika moja pale United iliposawazisha kupitia kwa nyota wake Chicharito, na hivyo kufanya timu hizo mbili kutoshana nguvu ya jumla ya magoli matatu kwa matatu bada ya dakika mia moja na Ishirini.

Mechi hiyo iliamuliwa kupitia mikwaju ya penalti na kwa mara ya kwanza, makipa wa timu hizo mbili waliokoa mikwaju kadhaa.

Kwa Ujumla mikwaju saba ziliokolewa au kupigwa nje na hivyo Sunderland kujikatia tikiti ya fainali dhidi ya Manchester City kwa magoli mawili kwa Moja.

Fainali ya kombe hilo itachezwa tarehe mbili Machi mwaka huu katika uwanja wa Wembley.

Post a Comment