MKURUGENZI WA HALIMASHAURI AKITOA TAARIFA
MWENYEKITI WA HALIMASHAURI KULIA AKISIKILIZA KWA MAKINI
BARAZA
MKRUGENZI WA HALIMASHAURI AKIFAFANUA JAMBO
DIWANI AKITAFAKARI JAMBO BAADA YA KUCHANGIA!
MADIWANI SERENGETI KWENYE KIKAO CHA BAJETI
KUWEKA KUMBUKUMBU SAWA
HALIMASHAURI
ya Wilaya ya Serengeti imepanga kufikia sifuri tatu katika mapambano
dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi kwa kutoa elimu ya
kutosha ambayo itamfikia kila mwananchi kuhusiana na athari za ugonjwa
huo.
Katika
taarifa yake kwenye kikao cha Baraza la madiwani cha kupokea,kujadili
na kupitisha mapendekezo ya mpango wa bajeti ya mwaka 2014-2015,Mratibu
wa Mpango wa Kudhibiti Ukimwi Wilaya ya Serengeti Elly Msamisa alisema
wamepanga kutoa elimu kwa njia mbalimbali ili kufikia mipango hiyo.
Alisema
elimu kuhusiana na masuala ya Ukimwi kwa jamii itatolewa kupitia
sinema,vikundi vya uelimishaji,kusimamia kwa karibu Kamati za Kudhibiti
Ukimwi ngazi ya Kata na Vijiji pamoja na kushirikiana na wadau wa
mapambano dhidi ya Ukimwi wilayani Serengeti.
Msamisa
alisema matarajio ni kufikia sifuri tatu ambazo ni maambukizi mapya ya
virusi vya ukimwi sifuri,vifi vitokanavyo na ukimwi sifuri pamoja na
ubaguzi na unyanyapaa wa waathirika wa ukimwi kufikia asilimia sifuri.
Alisema
kitengo cha kudhibiti ukimwi wilayani kimepanga kuimalisha mwitikio wa
jamii katika mapambano dhidi ya ukimwi,kupunguza hatari ya maambukizi
mapya katika sehemu hatarishi pamoja na kuimalisha uwezo wa kiuchumi kwa
makundi yanayoishi na virusi vya ukimwi na ukimwi.
Alidai
katika kipindi cha bajeti ya mwaka 2012-2013 kulikuwepo na changamoto
mbalimbali juu ya utekelezaji wa shughuli za mapambano dhidi ya ukimwi
kwenye kitengo cha kuratibu shughuli za
ukimwi na kufanya kazi kutokufanyika kwa usahihi.
Mratibu
huyo wa Ukimwi Wilaya ya Serengeti alisema baadhi ya changamoto hizo ni
ni idara za Halimashauri kutokuweka katika bajeti zao masuala ya ukimwi
na hata za kusaidia watumishi wanaoishi na virusi vya ukimwi katika
idara zao.
Akichangia
taarifa hiyo,Diwani wa Kata ya Manchila Michael Shaweshi alisema ili
Wilaya ya Serengeti itoke kwenye asilimia 4 ya maambukizi kimkoa
inapaswa kila Diwani kuwa na mipango ya kupambana na ukimwi wilayani
Serengeti.
Madiwani
wa Halimashauri hiyo kwa pamoja walipitisha bajeti ya mwaka 2014-2015
kiasi cha shilingi bilioni 31 ikiwa ni ongezeko kutoka bilioni 23
zilizopitishwa katika kipindi cha mwaka 2012-2013 ambazo zitafanya kazi
mbalimbali za kimaendeleo na miradi ikiwemo mapambano dhidi ya ukimwi
Post a Comment
0 comments