MAMBO YALIANZA NA KIKAO CHA WAJUMBE WA HALIMASHAURI KUU YA WILAYA
KADA WA CCM MZEE NYAKEKE
MBUNGE WA JIMBO LA RORYA LAMECK AIRO AKIZUNGUMZA
KULIA NI MWENYEKITI WA CCM MKOA WA GEITA JOSEPH MSUKUMA
KISHA UKAPIGWA MSOSI
TIMU YA UTEGI FF NA NYANDUGA FC ZIKIINGIA KWA AJILI YA MSCHEZO WA FAINALI AMBAPO TIMU YA UTEGI WALIIBUKA MABINGWA NA KUJINYAKULIA MILIONI TANO
UKAGUZI
MSUKUMA AKISALIMIANA NA MCHEZAJI WA UTEGI FC
SALAMU ZA FAIL PRAY NI MUHIMU KABLA MCHEZO KUANZA
MBUNGE AIRO GOLINI
MSUKUMA AKIENDA KUPIGA PENATI
HAPA BAO LILIFUNGWA
HAPA PENATI YA MWENYEKITI WA CCM RORYA NAMBA TATU ILIDAKWA
KIPA KUSHOTO MPIRA KULIA
FURAHA YA UBINGWA
AIRO AKIZUNGUMZA BAADA YA FAINALI
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitasita kuwasema na kuwafikisha kwenya
vikao vya maadili watumishi ambao watashindwa kufanya kazi zao na
kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama hicho na kupelekea kulalamikiwa na
Wananchi.
Akizungumza
katika mkutano wa maazimisho ya miaka 37 ya CCM wilayani
Rorya,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Geita Joseph Kasheku
‘Msukuma’alisema wataizingatia kauli ya Rais Jakaya Kiwete aliyoitoa
mkoani mbeya kutomuonea aibu mtumishi na kufatilia kwa karibu
utekelezaji wa ilani.
Alisema
kamwe hawatakubali kuona watumishi wazembe na wanaojiingiza kwenye
siasa kukwamisha shughuli za maendeleo kwa kutosimamia miradi huku
shutuma zikielekezwa kwa Serikali ya
CCM.
Msukuma
alisema katika siku za hivi karibuni kumeibuka taarifa za kuhusu Chama
cha Mapinduzi(CCM) wilayani Rorya kulalamikia utendaji kazi wa Mkuu wa
Wilaya hiyo pamoja na Mkurugenzi na kusema ili kazi ziweze kwenda ni
lazima viongozi wa CCM wawe wakali katika kusimamia ilani.
Mwenyekiti
huyo wa CCM mkoa wa Geita ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maazimisho
hayo yaliyofanyika kiwilaya katika uwanja wa Nyanduga,aliwataka viongozi
wa CCM Wilaya ya Rorya kutokusita kuzungumza kila wanapoona uzembe wa
watumishi.
"Niwashukuru
sana viongozi wa Chama Wilaya kwa kusimamia utekelezaji wa ilani na
kutokusita kuwazungumza viongozi ambao wanakwamisha shughuli za
maendeleo na kupelekea chama kulaumiwa.
"Mwenyekiti
wa Wilaya Samwer Kiboye"namba tatu,Mbunge Lameck pamoja na viongozi
wengine wa hapa Rorya muendelee na msimamo huo wa ufatiliaji wa
utekelezaji wa ilani na sisi tuko nyuma yenu hakuna haja ya kumuogopa
mtumishi yoyote asiyetekeleza majukumu yake",alisema Msukuma.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya Samwer Kiboye alisema
wapo watumishi ambao wamejiingiza katika siasa na kushindwa kufanya kazi
kutokana na taaluma yao ambao ndio kikwazo cha kufanya chama hicho
kulaumiwa.
Alisema
wapo watendaji ambao wanaanza kujadili Rais ajaye wakiwa ofisini na
kushindwa kutekeleza majukumu yao na kudai Rais ni mmoja Jakaya Kikwete
na hawata muonea haya mtumishi yoyote asiyewajibika.
Mwenyekiti
huyo alipongeza hotuba ya Rais kikwete aliyoitoa mkoani Mbeya katika
maazimisho ya miaka 37 ya CCM iliyowataka viongozi wa chama hicho
kuhakikisha wanafatilia kwa karibu utekelezaji wa ilani.
Kwa upande wa masuala ya michezo,Mbunge wa Jimbo la Rorya Lameck Airo alisema kila mwaka ataendelea kubolesha musuala ya michezo hususani kombe la Lamec ambapo kwa mwaka huu amedai kutumia zaidi ya milioni 30 ili kufanikisha mashindano hayo.
Alisema michezo licha ya kuwa nia ajira na kukuza vipaji pia anaitumia kama sehemu ya kuwaweka vijana pamoja na kushindwa kwenda kujiunga na makundi ambayo hayai katika jamii
Post a Comment
0 comments