0
 
MSHINDI WA BSS EMANUEL MSUYA BAADA YA KUPATA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50

 BEST NASSO KUTOA MPYA LEO BWALO LA POLISI
 ISAYA WA ADORINA ATAKUWEPO


Mshindi wa shindano la BSS 2013 Emanuel Msuya,msanii anayepanda juu kwa kasi Best Nasso pamoja na wasanii kibao wa mjini Musoma watapamba onyesho maalum la Valentine Day litakalofanyika leo kwenye fukwe za bwealo la polisi mjini Musoma.

Akizungumza na Blog hii,Mkurugenzi wa Kayombo Intertainment Docta Kayombo amesema maandalizi yote kuhusiana na show hiyo yameshakamilika na kinachosubiliwa ni wakatio kufika na watu kuvinjari kwenye fukwe hizo.

Amesema zoezi la kuuza kadi maalumu za show hiyo zimenunuliwa kwa wingi na wadau wa burudani mjini Musoma na kwa upande wa kampuni yake burudani wamejipanga ili kutoa burudani yenye kukidhi viwango.

Kayombo amesema ujio mpya wa kampuni ya burudani ya Kayombo Intertainment ina lengo la kukata kiu ya wapenzi wa burudani na kudai hilo litadhihirika leo kwenye show ya bwalo la polisi kuanzia saa 12 jioni.

Amesema mshindo wa BSS 2013 Emanuel Msuya usiku wa leo katika show ya wapendanao atazindua video ya wimbo wake usemao leo ni leo pamoja na nyimbo mpya huku msanii mwingine Best Naso anatarajiwa kutambulisha nyimbo zake mpya akiwa nyumbani na kusema weasanii wote wamejiandaa vizuri na watasindikizwa na wasanii wengine wengi wa musoma.

Docta Kayombo amesema licha ya wasanii hao,wappenzi wa burudani mjini musoma pia watarajie burudani kali ya show za madansa watakaochuana kuwania zawadi mbalimbali huku akitanabaisha wale watakaokuja wamependaza kwa vazi la valentine nao watapewa zawadi.

Kuhusiana na viingilio kwa wale ambao hawakubahatika kununua kadi kwa siku za nyuma,geti kwa wale watakaokuwa doble watalipa 6000 huku single wakilipa 5000 getini

Post a Comment