0
 WAKINAMAMA WAKIWA NA HUZUNI BAADA YA KUSIKIA MWANAMKE ALIYEFANYIWA UKATILI
 AFISA WA TAKUKURU MKOANI MARA AKITOA MSAADA KWA MWANAMKE ALIYEFANYIWA UKATILI
 FEDHA ZILIZOCHANGWA KUMSAIDIA MWANAMKE ALIYEFANYIWA UKATILI
 MENEJA KITENGO CHA MAENDELEO YA KANISA LA ANGLICANA JIMBO LA MARA DOCTA THEOPHIR KAYOMBO PIA ALIGUSWA NA MWANAMKE HUYO NA KUCHANGIA
 KATIBU TAWALA WA MKOA WA MARA BENEDICT OLE KUYAN AKIMPA MCHANGO WA FEDHA ZILIZOCHANGWA MWANAMKE ALIYEFANYIWA UKATILI MJINI BUNDA
KANISA la Anglicana Jimbo la Mara kupitia Kitengo cha Maendeleo ya Jamii wameahidi kusaidia kuchangia gharama za matibabu za Sumayi Girandi ambaye ni Mwanamke aliyefanyiwa ukatili wa kukatwa mkono na sehemu za siri na aliyedaiwa kuwa ni mume wake.

Meneja mradi wa Maendeleo ya Jamii wa Kanisa hilo docta Theophir Kayombo alitoa ahadi hiyo siku chache baada ya Mwanamke huyo kutoa ushuhuda wake katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani iliyofanyika kimkoa wilayani Bunda.

Alisema Kanisa liliguswa na ukatili mbaya aliofanyiwa Mwanamke huyo kwa kufuatwa nyumbani kwake usiku akiwa na watoto wake na kuanza kukatwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kupelekea kupoteza mkono wake mmoja wa kushoto na kuharibiwa jicho.

Kayombo alisema kutokana na rufaa aliyopewa Mwanamke huyo ya kwenda hospitali ya (KCMC) iliyopo Moshi Kanisa litatoa msaada wa karibu kuhakikisha anakwenda kufanyiwa matibabu ya kina ili kurekebisha jicho ambalo limeharibiwa na kumsababishia maumivu.

Alisema wameguswa na ukatili mbaya aliofanyiwa na kuona kuna umuhimu mkubwa kama sehemu ya jamii kuhakikisha wanakuwa karibu na muhanga huyo ili kutoa mchango wao katika kusaidia tatizo.

"Kwanza tunalaani ukatili huu aliofanyiwa Sumayi kwa kuvamiwa akiwa nyumbani kwake na huyo aliyekuwa mume wake na kushambuliwa vibaya kwa mapanga na kupoteza mkono wake wa kushoto na kuharibiwa jicho moja.

"Licha ya kupoteza mkono tulimsikia kwenye ushuhuda wake yakwamba aliandikiwa rufaa ya kwenda (KCMC)tutasaidia suala hilo lakini tunaaiomba jamii ibadilike na kuachana na matukio ya ukatili ambayo yanapoteza nguvu kazi ya Taifa.

Akitoa ushuhuda wa tukio hilo la kufanyiwa ukatili katika maazimisho ya siku ya Wanawake duniani mjini Bunda,Sumayi Girandi alisema usiku wa julai 4 mwaka 2013 akiwa nyumbani kwake katika Kijiji cha Kunzugu wilayani Bunda alivamiwa na aliyekuwa mume wake kabla ya kutengana na kumkata kwa mapanga.

Alisema aliyekuwa mume wake waliyetengana kutokana na tabia akiwa na mwenzake walimvamia ndani ya nyumba yake na kumkata sehemu mbalimbali za mwili wake na kupoteza mkono wa kushoto huku jicho moja likiwa limeharibiwa vibaya.

Sumayi alisema baada ya kupata matibabu katika hospitali ya DDH Bunda aliandikiwa rufaa ya kwenda (KCMC) kwa ajili ya oparesheni ya jicho linalomsumbua na kuwaomba wananchi kuweza kumsaidia ili kwenda kupata matibabu zaidi.

Post a Comment