WAKATI
uchaguzi wa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalumu la Katiba ukitarajiwa
kufanyika leo jioni mjini Dodoma, tayari wagombea wawili waliojitokeza
kuchukua fomu ya kutaka kuwania nafasi hiyo, wameenguliwa baada ya
kushindwa kurudisha fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa muda uliopangwa.
Wajumbe
hao ni pamoja na Dkt. Theresya Huvisa pamoja na Danstan Chipaka
wameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho kufuatia kushindwa kurudisha
fomu za kugombea ambazo zilipaswa kurudishwa leo saa 4 asubuhi.
Kufuatia
kuenguliwa kwa wajumbe hao, nafasi hiyo sasa itawaniwa na Samwel Sitta
pamoja na Hashim Rungwe, ambao ndiyo waliokidhi vigezo kwa kuchukua
fomu na kurudisha kwa wakati.
Uchaguzi
wa Mwenyekiti unatarajiwa kufanyika leo saa 10 jioni, ambapo baada ya
kutangazwa matokeo kutatangazwa uchukuaji fomu kwa wajumbe watakaotaka
kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, ambaye kulingana na kauli za
mwenyekiti wa muda aliyepita kuzingatia 'Jenda' atakuwa ni mwanamke.
Mpaka sasa anayetajwa kutarajiwa kuwania nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti, ni Samia Suruhu.
Kwa
mujibu wa kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Makamu Mwenyekiti wa Bunge
anapaswa kutoka upande wapili wa muungano iwapo Mwenyekiti atakuwa
amechaguliwa kutoka upande mwingine wa muungano ili kuleta usawa.
Post a Comment
0 comments