MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA AKIFUNGUA MKUTANO HUO
WADAU WA AFYA WAKIFATILIA
UMAKINI UNAHITAJIKA ILI KUJADILI KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA WAJAWAZITO WA WATOTO WACHANGA
MKURUGENZI WA SHIRIKA LA EVIDENCE FOR ACTION CRAING FERLA AMBAYE SHIRIKA LAKE NI MDAU MKUBWA WA KUPUNGUZA VIFO VYA AKINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO WACHANGA
WADAU WAKIWA KWENYE MKUTANO WA PAMOJA
BAADA YA MKUTANO
FERLA AKIJADILIANA JAMBO NA MKUU WA MKOA WA MARA
KUKOSEKANA kwa uhadilifu kwa baadhi ya wauguzi na wataalamu wa afya
katika zahanati,vituo vya afya na hospitali mkoani Mara imeelezwa ndio chanzo
cha kupelekea vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa
wa Mara JohnTuppa alipokuwa akifungua kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji mpango mkakati wa kupunguza vifo vya akina
mama wajawazito na watoto wachanga mkoani Mara katika kipindi cha julai 2013 hadi
januari 2014.
Amesema wananchi wengi wamekuwa
wakitoa malalamiko kuhusu kukosekana kwa uhadilifu, maadili ya kazi na uaminifu
na kupatikana kwa huduma mbovu ambazo zimekuwa zikipelekea matatizo kwa akina
mama wajawazito na kupelekea vifo vyao na watoto wachanga.
Mkuu wa mkoa huyo amesema changamoto
hiyo pamoja na nyingine ambazo zimekuwa chanzo cha vifo hivyo inapaswa
zifanyiwe kazi na kila mmoja mwenye dhamana kwa kutimiza wajibu wake na
kuwataka wakuu wa Wilaya kuwa waangalizi na wafatiliaji katika suala hilo.
Amesema mkoa wa Mara hauwezi
kukubali kuona vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga vikiendelea
kutokea kutokana na uzembe wa watu wachache kushindwa kutoa huduma zifaazo za
afya.
Amesema ili kufikia lengo kusudiwa mkoa
huo utatekeleza malengo mahususi likiwemo lengo la kusajili wanawake wajawazito na
kuwafuatilia ili kuhakikisha wanahudhulia kliniki na hata wakati wa
kujifungua wanakwenda kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma vya afya sambamba na kuongeza vifaa tiba.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mkakati wa nkoa
kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga mkoa wa
Mara,mganga mkuu wa mkoa Samson Wenani amesema ili kuhakikisha huduma
bora zinasogezwa karibu uboreshaji vituo 13 vya afya kwa kujenga majengo
ya upasuaji na kuweka vifaa tiba kwa ajili ya kuwasaidia wajawazito
wanakwenda kujifungua.
Amesema majengo ya upasuaji pamoja na nyumba za madaktari
wakuwasaidia wajawazito yamejengwa katika vituo vya afya vya
Nyasho,Murangi,Kyagata,Iramba,Natta,Ikizu,Kasahunga,Kinesi,Muriba na
Nyarwana ambapo kazi za ukamilishaji wa majengo yote katika maeneo hayo
inatarajiwa kukamilika mwezi machi mwaka huu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Evidence For Action Craig Ferla ambaye kupitia shirika hilo wanaosaidia mkakati wa mkoa wa Mara kupunguza vifo hivyo alisema anashukuru mkoa kwa kudhamilia kwa dhati kuhakikisha wanapunguza na kumaliza kabisa vifo vua akina mama wajawazito na watoto wachanga ambavyo vimeonekana kutokea kwa wingi mkoani Mara.
Post a Comment
0 comments