HALIMASHAURI
Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Butiama imetoa tamko la
kuikataa kampuni ya ujenzi ya (CMG)inayomilikiwa na Mjumbe wa NEC Taifa
Christopher Gachuma kwa kushindwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa bwawa
la umwagiliaji.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mara baada ya Kikao cha Mkutano Mkuu,Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Butiama Yohana Mirumbe amesema kampuini hiyo imeshindwa
kutekeleza mradi kwa wakati huku kazi ikiwa bado kubwa na hivyo
kuwakwamisha wananchi.
Amesema
mradi huo uliopo kwenye Kijiji cha Masinono Kata ya Bugwema kukamilka
kwake kungewapa nafasi kubwa wananchi kufanya kilimo cha umwagiliaji na
kuepukana na matatizo ya njaa kila mwaka lakini mkandarasi huyo
ameshindwa
kwenda na wakati.
Mirumbe
amesema Chama cha Mapinduzi hakitashindwa kuchukua hatua na kuzifikisha
sehemu husika kwa mkandarasi yoyote ambaye atashindwa kukamilisha mradi
huku chama hicho kikitupiwa lawama na wananchi.
Amesema
mkutano mkuu wa Chama hicho umeikataa kampuni ya Gachuma ya (CMG)
kuendelea na mradi huo na kuiomba Wizara ya Kilimo na Chakula ambayo
ndio iliyopitisha zabuni ya kampuni hiyo kufatilia suala hilo na
kuiondoa.
Mwenyekiti
huyo amesema mara kadhaa viongozi wa mkoa na chama wamekuwa
wakiwasiliana na mkandarasi huyo juu ya kukamilisha mradi huo lakini
ameshindwa kusikiliza na sasa hawawezi kuonea yoyote aibu bali wanataka
utekelezaji wa ilani inatekelezwa.
Awali
akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika sekta
ya umwagiliaji,Mkuu wa Wilaya ya Butiama Angelina Mabula amesema ujenzi
wa mradi wa umwagiliaji katika kijiji cha Masinono umekuwa wa kusuasua.
Amesema mradi huo ulio chini ya DASIP uliofadhiliwa
na benki ya Dunia ulitengewa bilioni 1.2 na tayari ulianza utekelezaji
wake tangu mwanzoni mwa mwaka 2013 lakini mkandarasi bado amekuwa nyuma
kiutekelezaji.
Post a Comment
0 comments