0
 
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameunda kamati ya watu tisa kuratibu maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF ilipojiunga na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
TFF ilipata uanachama wa shirikisho hilo la kimataifa Oktoba 8, 1964 ambapo itaadhimisha miaka hiyo 50 kwa kufanya shughuli mbalimbali za mpira wa miguu.
Kamati hiyo itaongozwa na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya magazeti ya Serikali, Gabriel Nderumaki wakati Katibu atakuwa Lina Kessy ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Wanawake (TWFA).
Wajumbe ni Ahmed Mgoyi, Hoyce Temu, Teddy Mapunda, Ruge Mutahaba, Richard Kasesela, Boniface Wambura na Meneja Biashara wa TFF anayetarajiwa kuajiriwa hivi karibuni.
Kamati itafanya kikao chake cha kwanza Jumatatu (Machi 3 mwaka huu) kwenye hoteli ya Courtyard iliyopo Upanda Seaview saa 7 mchana.

Post a Comment