0

JESHI la polisi mkoani Mara linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Kemoramba wilayani Butiama Marwa Boniphace (16) kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa mwaka 1 na miezi 10.
 

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Paul Kasabago amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 13 majira ya saa 9:00 mchana alipokuwa rikizo kwa kaka yake mjini Musoma baada ya shule kufungwa.

 
Kasabago amesema  tukio hilo lilitokea katika  mtaa wa Nyankanga Kata ya Makoko mjini Musoma baada ya kuachiwa mtoto huyo na shemeji yake aliyekuwa ameenda kuchota maji ramboni(bwawa).
 
Amesema baada ya mama wa mtoto huyo kurudi alimkuta mtoto wake akiwa katika hali mbaya na alipomchunguza mwanae alimkuta kaharibika sehemu za siri huku mguu wa kushoto ukionekana kuwa na itilafu kama kuvunjika nyonga.
 
Kwa upande wake mama wa mtoto huyo Annabeli Waitara(24) alipokuwa akisimlia mkasa huo nje kidogo ya Kanisa la Anglicana mjini Musoma amesema  kijana huyo ni shemeji yake kwa maana ya kwamba ni mdogo wa mume wake.
 
 Annabeli amesema katika ndoa yake ana muda wa miezi mitatu,na mtoto huyo sio mtoto wa mwanaume  aliyemuoa bali ameolewa tayari akiwa na mtoto huyo na kudai kusikitishwa na tukio lililofanywa na shemeji yake kutokana na umri wa mtoto huyo. 

Kufuatia tukio hilo,Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya kijamii la (Jamii Information Network) Augustine Mgendi amedai kusikitishwa na tukio hilo na kuviomba vyombo vya dola licha ya umri wa mtuhumiwa ufanyike uchunguzi makini kuhusiana na tukio hilo na pale itakapobainika amefanya tukio hilo hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Amesema ni kitu cha ajabu kufanya tukio la namna hiyo kwa mtoto wa mwaka 1 na miezi 10 ambalo licha ya kustaajabisha linatia uchungu kuona mtoto wa umri huo kufanyiwa kitendo hicho na kudai shirika lake lina laani tukio hilo na kuitaka jamii kubadilika na kuachana na matukio ya ajabu kama hayo.

Post a Comment