TUME ya Uchaguzi nchini (NEC) imeomba ushirikiano kwa Vyombo
vya Habari katika zoezi kuhusu maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura litalitakaloanza hivi karibuni kwa kuhamasisha jamii umuhimu wa
kujiandikisha kwenye daftari hilo.
Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari mjini Musoma,Kamishina wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mchanga Mjaka amesema kutokana na umuhimu wa
Waandishi wa Habari,Tume hiyo imeona ni vyema kuanza nao ili waweze kupata
elimu na baadae watumie nafasi yao kuhamasisha Wananchi kwa kuandika Habari na Makala
ili kushiriki kwenye zoezi hilo muhimu.
Amesema Wahariri na Waandishi wa Habari wana mchango mkubwa
kuhamasisha wananchi na kupata taarifa ili waweze kwenda vituoni na
kujiandikisha kwaajili ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na upigaji kura ya maoni
ya kupata Katiba mpya hivyo ni vyema
wananchi wakatambua umuhimu wa zoezi hilo kwa sasa.
Mjaka amesema katika uboreshaji wa daftari hilo,wapiga kura
wote waliojiandisha awali na wale wapya watalazimika kwenda kituoni kwaajili ya kuandikishwa upya kwa maana ya
kuchukuliwa taarifa za kibailojia (Biometric Features).
Amesema ili zoezi hilo liweze kufanikiwa kwa malengo
yaliyokusudiwa,kwa kiwango kikubwa Tume inategemea vyombo vya Habari kutokana
na uwezo na hekima ya kuhamasisha jamii na wananchi kupitia vyombo mbalimbali.
Kamishina huyo wa Tume ya Uchaguzi alisema kwa kuwatumia
Waandishi wa Habari wataweza kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika
vituo vya kujiandiskisha mara baada ya Tume ya Uchaguzi itakapovitangaza muda
utakapo wadia.
Post a Comment
0 comments