BAADHI YA VIJANA WA JIJI LA MWANZA WAKIWA KATIKA UFUNGUZI WA KAMPUNI YA BEGA KWA BEGA MICROFINANCE.
Vijana
nchini wameshauriwa kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika maeneo yao
ili waweze kumiliki rasilimali zilizopo na kumiliki uchumi wa nchi.
Kauli
hiyo imetolewa jijini mwanza na afisa maendeleo ya jamii damas mkama
wakati akifungua huduma ya utoaji wa mikopo kwa kampuni ya bega kwa
bega microfinance
Akizungumza
kwa niaba ya fisa maendeleo wa jiji afisa vijana juma samweli amesema
hatua hiyo itawasaidia kujiimalisha kiuchumi kwa maisha yao ya sasa na
baadaye.
Kwa upande
wake afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya bega kwa bega microfinance
albert girenga amesema kuwa lengo la kampuni hiyo ni kuwawezesha vijana
wenye ujuzi na wasio na ujuzi kuweza kujiajili.
Amesema kuwa lengo hilo litafikiwa kupitia mikopo itakayotolewa na kampuni hiyo kupitia mikopo ya anzisha na imarisha.
VIJANA WAKIENDELE KUJIFUNZA.
Awali
mkurugenzi wa ubunifu na ugunduzi kutoka kampuni ya godtec aloyce
midelo amesema kuwa nia ya godtec ni kuinua kipato cha mwananchi wa
hali ya chini kupitia huduma ya uwezeshaji wananchi kiuchumi (poso)
Musa
magari ni muuzaji wa bidhaa za mitumba amesema kuwa ukopaji wa vikundi
umechangia kuwarudisha nyuma baadhi ya wafanyabishara kutoka na baadhi
ya watu kutokuwa waaminifu.
UMAKINI ULICHUKUA NAFASI SANA KATIKA UZINDUZI HUO.
Post a Comment
0 comments