0


KADA wa Chama cha Mapinduzi(CCM) aliyetangaza nia ya kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho,Profesa Sospeter Muhongo,kesho anatarajia kukamilisha zoezi la kusaka wadhamini akiwa mjini Musoma kama alivyoahidi kumalizia wakati akitangaza nia yake hivi karibuni.Kwa mujibu wa kamati inayoratibu na kusaidia shughuli za Profesa Muhongo,zoezi la kudhaminiwa kada huyo,litaanza kufanyika kuanzia majira ya saa3 asubuhi katika ofisi za CCM wilaya ya Musoma zilizopo eneo la bus stop na Nyasho.Kamati hiyo imewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliokusudia kumdhamini profesa Muhongo,kufika mapema kwenye ofisi hizo ili zoezi la udhamini liweze kukamilika kwa muda uliopangwa na kuzingatia ratiba.

Kabla ya kupokea fomu za udhamini kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ya Musoma,Profesa Muhongo atasaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za CCM mkoa zilizopo maeneo hayo na baadae kutoa shukrani kwa wale waliojitokeza kumdhamini.

 PICHA NI MATUKIO WAKATI AKITANGAZA NIA YA KUGOMBEA NAFASI YA URAIS


Post a Comment