WATOTO watatu wa familia moja katika Kitongoji cha
Machawa, Kijiji cha Malonga Kata ya Milale wilayani Rorya, mkoani Mara,wameteketea kwa moto baada ya kuungulia ndani ya nyumba.
Tukio hilo lilitokea juzi mapema alfajiri
mara baada ya mama mzazi wa watoto wawili kati ya watatu waliopoteza maisha,kuwaacha
ndani wakiwa wamelala na kwenda katika maeneo ya mto ulio jirani na nyumbani kwaajili
ya kununua mboga.
Watoto waliofariki dunia kutokanana tukio
hilo ni Baraka Godfrey na Happy Iddi wenye umri wa miaka 3 kila mmoja na Bella
Godfrey mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.
Shuhuda wa tukio hilo,Elisha
Mugha,aliuambia mtandao huu,alishuhudia moshi ikitoka kwenye nyuma hiyo ndipo ndipo
alipotoa taarifa kwa majirani wengine waliokuwa jirani na nyumba hiyo na kuamua
kwenda kutoa msaada wa kuuzima moto huo.
Alisema walipofika eneo la tukio
walianza kuuzima moto huo na mara ulipo pungua walishuhudia kuwepo kwa watoto
watatu wakiwa tayari wameshapoteza maisha kwa kuungua na moto huo.
“Hatukujua kama kulikuwa na watoto
ndani,tuliwaona baada ya moto kupungua na kuwatoa ndani wakiwa tayari
wameshapoteza maisha baada ya kuungua vibaya kutokana na kukosa msaada wa
haraka.
“Baada ya kuwatoa tuliwahifadhi
kwenye jiko la kupikia lililokuwa jirani na wakati wote ambao tulikuwa kwenye
nyumba hiyo mama wa watoto hao alikuwa bado hajarudi,”amesema shuhuda huyo
Kamanda wa jeshi la polisi kanda
maalumu ya Tarime/Rorya,Lazaro Mambosasa,alisema taarifa kamili ya chanzo cha
moto uliosababisha vifo vya watoto hao bado hakija julikana huku upelelezi wa
kubaini chanzo chake ukiwa bado unaendelea.
Kufuatia tukio hilo,kamanda huyo
ametoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano wa kubaini chanzo cha moto huo na
kuwataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya moto ambayo yamekuwa
yakisababisha vifo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
wilayani Rorya,Samweri Kiboye,ametoa misaada ya kibinadamu kwa familia hiyo
ikiwemo vyakula,godoro,nguo,shuka,branketi,sabuni,chumvi,mchele pamoja na kiasi
cha shilingi laki moja ili kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu kwa familia
hiyo.
Post a Comment
0 comments