0
 CHAMA cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Musoma mjini,leo kimefanya mkutano mkubwa wa kampeni wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata mpya ya Mshikamano ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake katika kuhakikisha inashinda kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba kwa nafasi za udiwani,ubunge pamoja na Rais.

Akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kusikiliza mkutano huo,mgombea udiwani wa Kata hiyo,Charles Mwita,amesema kutokana na heshima waliomuonyesha wananchi kwa kujitokeza kwa wingi,atahakikisha anawalipa maendeleo pale atakapofanikiwa kushinda kwenye uchaguzi oktoba 25.


Amesema umati huo umedhihilisha imani kubwa juu yake na kudai kero za Kata hiyona changamoto zake tayari ameshazibaini na atahakikisha pindi atakapochaguliwa atakuwa ni diwani wa vitendo na sio udanganyifu.

Mwita amesema imani waliomuonyesha kwenye mkutano huo waendelee kumuonyesha hadi ifikapo oktoba 25 kwa kumpigia kura za kishindo pamoja na mgombea urais John Pombe Magufuli na mgombea wa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo.

Akizungumza kwenye mkutano huo,Katibu wa CCM wilaya ya Musoma mjini,Jacob Nkomola,amesema wananchi wamechoka kudanganywa na sasa wameamua kukiamini chama hicho na hilo limekuwa likijihidhilisha kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano.


Amesema mkutano wa kesho utakaofanyika Kata ya kwangwa,utahudhuliwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma mjini na kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kusikiliza sera za chama hicho na kufanya maamuzi sahihi oktoba 25.



 MRS.MWITA AKIOMBA KURA ZA MZEE
 





 MWITA AKIOMBA KURA KWA WANANCHI


Post a Comment