Makamu wa
Rais aliwaomba viongozi wa dini zote nchini kuombea amani na kuhamasisha
waumini wao kujitokeza kupiga kura oktoba 25 ili kutekeleza haki ya kikatiba na
kuwasihi kukataa kushawishika na vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kuhatarisha
amani kwa kudai pasipo na amani hakuna maendeleo.
“Napenda kuwakumbusha kwamba mwaku huu ni mwaka wa
uchaguzi na hivi sasa kampeni
zinaendelea kila kona ya nchi kwa wanasiasa kujinadi kwa wapiga kura kuomba ridhaa
ya wananchi kwenye uchaguzi utakaofanyika oktoba 25.
“Rai yangu
kwa watanzania wote,nawakumbusha kulinda amani,umoja na mshikamano wa taifa
letu kwa nguvu zetu zote na kwamba tofauti za dini,itikadi za siasa,rangi na
makabira yetu yasiweze kutugawa na kila tunalolifanya tutangulize mbele masrahi
ya taifa.
“Napenda
kuwahakikishia,sisi ndani ya serikali tumejipanga vilivyo kuhakikisha uchaguzi
mkuu unafanyika kwa amani na utulivu kwa kusimamia uchaguzi huru na haki kama
ambavyo imekuwa ikizungumza kuanzia mwanzo wa mchakato huu,”alisema.
KAIMU MUFTI WA TANZANIA,SHEK HAMID JONGO AKIENDESHA SWALA UWANJA WA SHULE YA MSINGI MUKENDO
WAUMINI WAKISIKILIZA MAWAIDHA
Post a Comment
0 comments