MAKAMU wa Rais,Dkt.Mohamed Gharib
Bilal,amewasili mjini Musoma kuungana na waumini wa dini ya kislamu katika
swala ya sikukuu ya Idd al Hajj inayofanyika kitaifa mkoani Mara siku ya kesho.
Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
ndege wa Musoma,alikwenda kusaini kitabu chawageni kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa
wa Mara na kasha kuelekea kwenye ofisi
za Baraza la Waislamu mkoa wa Mara(Bakwata) na kukutana na viongozi wa dini ya
kiislamu.
Akizungumzia na BINDA NEWS kuhusiana
na maandalizi,Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya waislamu mkoa wa Mara,Said
Gantala,alisema maandalizi kuhusiana na ibada hiyo ambayo huadhimishwa duniani
kote baada ya kumalizika kwa Hijja yamekwisha kukamilika yakiwemo maandalizi ya
harambee hiyo.
Amesema baada ya kumalizika kwa
swala itakayoswaliwa kwenye viwanja vya shule ya msingi mkendo kuanzia saa 2
kamili,kuanzia mchana kutafanyika Baraza
la Idd litakalofanyika kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania tawi la Mara
ambapo pamoja na mambo mengine yatakayozungumzwa kutafanyika harambee kwaajili
ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Ijumaa wa mkoa wa Mara.
Gantala amesema harambee hiyo
inafanyika kutokana na Msikiti ambao umekuwa ukitumika kwa muda mrefu kama
Msikiti mkubwa unaotumiwa na watu wengi kuwa na nafasi ndogo pamoja na kuchaka
kwa miundombinu yake.
Amesema katika kuweza kufanikisha
ujenzi wa msikiti huo wa kisasa,kiasi cha shilingi bilioni 1.5 zinahitajika na
wametoa mialiko ya kushiriki kwa waumini wote wa dini ya dini pamoja na
viongozi mbalimbali ili kuweza kufanikisha shughuli hiyo.
Amesema ujenzi wa msikiti ni sadaka
yenye kudumu na malipo yake yatapatikana siku ya hukumu mbele ya Mwenyezi Mungu
hivyo kutoa wito kwa kila mmoja kuona umuhimu wa kushiriki kwenye ujenzi wa
nyumba ya ibada.
Idd al Hajj, husheherekewa kama
kumbukumbu ya sadaka ya Ibrahimu ambaye kufuatana na taarifa za Qurani
alikuwa tayari ya kumchinja mwanawe kama sadaka kwa Mungu lakini Mungu alimzuia
asimchinje akampatia kondoo badala yake, Qurani sura al-Hajj aya 37.
Post a Comment
0 comments