MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
Chama cha Mapinduzi (CCM)John Pombe Magufuli,amemaliza kwa kishindo kampeni
zake mkoa wa Mara kwenye uwanja wa shule ya msingi mkendo huku uwanja huo
ukivunja rekodi kwa kujitokeza maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza na
kudai kutokana na imani kubwa waliomuonyesha kwa kujitokeza kwa wingi hawezi
kuwaangusha iwapo ataunda serikali.
Kabla ya kuhitimisha uwanjani hapo,Magufuli amefanya
mikutano ya kampeni kwenye majimbo matano ya uchaguzi yakiwemo ya Tarime
vijijini,Tarime mjini,Rorya,Butiama na Musoma vijijini ambapo katika mikutano
yote watu wengi walijitokeza kumsikiliza na hakushindwa kuongelea vipaumbele
vyake ikiwemo suala la wanafunzi kusoma bure kuanzia elimu ya msingi hadi
kidato cha nne.
Akiwa kwenye uwanja wa mkendo,Magufuli alisema amefarijika
sana na umati mkubwa wa watu walijitokeza na kuahidi kutimiza maombi
yaliyotolewa na mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo juu ya
ujenzi wa barabara za kiwango cha lami kwenye barabara za mjini na pembezoni
pamoja na kupeleka kwa kasi ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwalimu Nyerere
iliyopo Kwangwa ili wananchi wapate huduma bora ya afya.
Alisema kutokana na imani waliyomuonyesha anaamini wanampa
kura za kutosha pamoja na kumchagua Mathayo ili aweze kusukuma mbele maendeleo
ambapo pia aliwaombea kura madiwani wanaotokana na CCM.
Baada Ya kumaliza ziara mkoani Mara,kesho Magufuli
anatarajia kuendelea na kampeni mkoa wa Simiyu katika Jimbo la Busega.
Sehemu ya umati wa wananchi
Wakeleketwa wa CCM
Mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo akizungumza kwenye mkutano huo
Makongoro Nyerere na Mwigulu Nchemba
Post a Comment
0 comments