0
MGOMBE urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi,Docta,John Pombe Magufuli,amewasili leo mkoani Mara na kufanya mikutano mikubwa ya kampeni kwenye majimbo matatu kati  ya majimbo 10 ya mkoa wa Mara nakuwaomba kura wananchi huku akiomba aaminiwe na kuchaguliwa kwa kuwa hatawaangusha watanzania.

Baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Musoma majira ya saa 5 asubuhi,Magufuli alielekea Butiama na kuweka shada la maua kwenye Kaburi la Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere kabla ya kufanya mkutano wa hadhara na kuwaombea kura wagombea ubunge jimbo a Butiama kwa mgombea wake Nimrod Mkono pamoja na Jimbo la Musoma vijijini alogombea Profesa Sospeter Muhongo na madiwani wanaotokana na CCM.

Katika Wilaya ya Bunda uwanja wa sabasaba ambao ulijaa watu wengi waliojitokeza kumsikiliza,Magufuli aliomba kura na kuwaombea wagombea ubunge majimbo ya Bunda mjini na Mwibara yanayogombewa na Stephine Wasira na Kangi Lugora kabla ya kuelekea Jimbo la Bunda vijijini ambapo pia alimnadi mgombea wa Jimbo hilo,Boniphace Mwita.

Magufuli amerejea Musoma mjini na kesho ataendelea na kampeni kwenye majimbo mengine ya mkoa wa Mara ambapo jioni atahitimisha kwa kufanya mkutano kwenye uwanja wa shule ya msingi mkendo kabla ya kuendelea na ziara mkoa wa Simiyu.


 Wananchi wa Manispaa ya Musoma wakimsubili Magufuli uwanja wa ndege kabla hajafika
 Magufuli akimshukuru rubani baada ya kutua salama uwanja wa ndege Musoma
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Christopher Sanya akimkaribisha Magufuli
 Mgombea ubunge wa Jimbo la Musoma mjini,Vedastus Mathayo,alikuwepo kwaajili ya kumpokea magufuli
 magufuli akiangalia vikundi vya burudani
 magufuli akizungumza na Chief Wanzagi wa Butiama
 Hapa akiweka shada la maua kwenye Kaburi la Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere
 Chief akimkabidhi fimbo kwa niaba ya wazee wa Butiama
 Wananchi wakifatilia mkutano wa Butiama
 Hapa ni uwanja wa sabasaba Bunda

 akimnadi Wasira na Kangi Lugora
 Picha ya chini mkutano wa Nyamswa Jimbo la Bunda Vijijini

Post a Comment