0

 MGOMBE ubunge wa Jimbo la Tarime mjini,kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Esther Matiko,amezindua kampeni zake za kuwania jimbo hilo na kudai moja ya kipaumbele chake ni suala la elimu na kudai iwapo hilo litafanikiwa masuala mengine yataweza kufanyika.
Alisema haiwezekani wanafunzi wa shule tatu wanasoma kwenye shule moja kwa kupokezana muda wa kuingia darasani huku hali hiyo ikiangaliwa na viongozi walipita na kushindwa kuwafanya wanafunzi kukosa elimu stahiki.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo,Esther,alisema Jimbo la Tarime linazo changamoto nyingi ambazo Chama cha Mapinduzi kimeshindwa kuzitatua na sasa wananchi wanazo sababu za kukipumzisha kuanzia nafasi ya ubunge,udiwani hadi urais.

Alisema vipaumbele vikubwa vitatu vya elimu,afya na uchumi kwa wananchi wa Tarime amekusudia kuvifanyia kazi mapema ili elimu bora iweze kupatikana kwa wanafunzi,afya bora pamoja na kuona wananchi wanaondokana na umasikini kwa kubuni njia mbalimbali za kujiwezesha kiuchumi.

“Nilikuwa Mbunge wa viti maalumu kwenye bunge lililopita lakini nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuwzungumzia wananchi wa Tarime wakati mbunge wa Jimbo alikuwepo na alikuwa akikaa kimya kule bungeni.

“Nimekuja kuwaomba ili niingie bungeni kutokea kwenye Jimbo ili niweze kuwa na nafasi kubwa ya kuweza kuzungumzia masuala mbalimbali ambayo yanatuhusu  hapa jimboni na kuweza kuyapatia utatuzi,”alisema.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda mjini,Esther Bulaya,aliwaomba wananchi wa Tarime wasifanye kosa tena bali ifikapo oktoba 25 wampigie kura za kutosha Esther Matiko, ili aweze kuwaletea mabadiliko ya kweli.
 Burudani pia zilikuwepo
 wananchi wakishangilia mkutano

 Esther Matiko kulia,akiwa na mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Tarime na kushoto ni Esther Bulaya
 Esther Bulaya akimuombea kura esther matiko

 Esther akipokea kitabu cha ilani ya Jimbo
 hapa akiwa na familia yake
 akiwahutubia wananchi

 sehemu ya wasikilizaji


Post a Comment