0MJUMBE WA TIMU YA KAMPENI ZA CHAMA CHA MAPINDUZI,MWIGULU NCHEMBA,LEO ATATUA MJINI MUSOMA KWA KUTUMIA “CHOPA”TAYARI KUOMBA KURA KWA WAGOMBEA WA CHAMA CHA MAPINDUZI KUANZIA NGAZI YA URAIS,UBUNGE PAMOJA NA UDIWANI MKUTANO AMBAO UTAFANYIKA KATA YA IRINGO KUANZIA SAA 8 MCHANA AMBAPO MKUTANO HUO UTAHUDHURIWA PIA NA MGOMBEA UBUNGE WA JIMBO LA MUSOMA MJINI,VEDASTUS MATHAYO.
AKIZUNGUMZA NA BLOG HII,KATIBU WA SIASA ITIKADI NA UENEZI WA CCM,RAMADHANI CHACHA(MUSOMA BUS) ALISEMA MIKUTANO YA KAMPENI KATIKA JIMBO LA MUSOMA MJINI INAENDELEA VIZURI NA KUWAOMBA WANANCHI WOTE BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA,KUJITOKEZA KWENYE MKUTANO HUO ILI KUSIKILIZA NINI KINACHOSTAHILI KUFANYIWA WANANCHI WA JIMBO LA MUSOMA MJINI NA TANZANIA KWA UJUMLA.

KATIBU WA CCM WILAYA YA MUSOMA MJINI NI KAMA ANASEMA"MUDA NDIO HUU"
 


Post a Comment