0


MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA MARA,KAPTENI MSTAFU,ASERI MSANGI,AMEWATAKA WANANCHI KUTOKUOGOPA KUJITOKEZA KUPIGA KURA KWA KUWA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VIMEJIPANGA ILI KUHAKIKISHA KILA MMOJA ALIYEJIANDIKISHA KUPIGA KURA ANAPATA HAKI YAKE YA KUPIGA KURA.

AKIZUNGUMZA NA ASKARI WA VIKOSI VYA MAJESHI MBALIMBALI VILIVYOSHIRIKI MAZOEZI YA PAMOJA KUJIANDAA NA MAMBO MBALIMBALI YAKIWEMO YA ULINZI WAKATI WA UCHAGUZI,MSANGI AMBAYE PIA NI MKUU WA MKOA WA MARA,ALISEMA WANANCHI HAWANA SABABU ZA KUWA NA HOFU NA WAJIANDAE KWAAJILI YA ZOEZI LA UPIGAJI KURA.

ALISEMA MAZOEZI YA PAMOJA YA ASKARI YAMEMKUMBUSHA MBALI WAKATI AKISHIRIKI VITA VYA KAGERA MWAKA 1979 NA KUWATAKA ASKARI KUZINGATIA MAADILI WAKATI WA KUTIMIZA MAJUKUMU YAO WAKATI WAKISIMAMIA ZOEZI LA UCHAGUZI.




 ASKARI WAKIFANYA MAZOEZI YA PAMOJA





Post a Comment