0
 
 MKUU wa mkoa wa Mara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama,Magesa Mulongo,ametoa muda wa wiki 3 kwa wananchi  wote wanaomiliki siraha kinyume cha Sheria kuzisalimisha polisi au kwa kiongozi yoyote kuangazia ngazi ya Kijiji kabla ya oparesheni kali kuanza ya kuwasaka na kuwachukulia hatua watu wote wanaomiliki siraha hizo.
 Akizunguumza na wakuu wa wilaya,wakurugeinzi na wenyeviti wa Halimashauri za mkoa wa Mara,Mulongo alisema zoezi hilo litawahusu wanaomiliki kinyume cha Sheria na wale wanaomiliki kihalali ili kuangalia uhalali wao wa kumiliki siraha kwa kuwa wapo ambao wanazitumia kinyume na mkataba wa umiliki wa siraha uliokuwepo kabla ya kuanza kuimiliki.
 Mulongo alisema mkoa wa Mara kwa sasa lazima uangalieika kuwaletea maendeleo wananchi kutokana na rasilimali zilizopo na sio kushughulikia matukio ya ujambazi unaotokana na matukio ya kutumia siraha.
 Mkuu wa mkoa wa Mara akiiagana na viongozi wa mbalimbali wa mkoa wa Mara wakiwemo wakuu wa wilaya mara baada ya kumaliza kikao chake kwenye ukumbi wa mikutano wa mkuu wa wilaya ya Bunda

Post a Comment