0
Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) sasa itaanza Jumamosi Mei 9, 2015 badala ya Jumamosi Mei 2, 2015 kama ilivyokua imetangazwa awali.

Uamuzi huo umefanyika ili kutoa fursa kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukamilisha maandalizi ya mwisho ikiwemo ukaguzi wa viwanja.

Wakati taarifa hiyo ikitolewa na TFF,mabingwa wa soka mkoa wa Mara timu ya Igwee fc,wameendelea kujifua ili kujiweka vizuri na ligi hiyo katika kuhakikisha inafanya vizuri huku wito ukitolewa kwa wachezaji mbalimbali kufika kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye uwanja wa posta mjini Musoma.

Post a Comment