0
 
MFUKO wa Pensheni wa (PSPF) mkoa wa Mara,umewakumbusha walimu watarajiwa ambao ni wanachuo cha uwalimu katika vyuo vya  Musoma Utalii na Mtakatifu Alberto,vilivyopo manispaa ya Musoma kujenga utaratibu wa kijiwekea akiba hata kabla hawajapata ajira rasmi katika sehemu mbalimbali mara baada ya kuhitimu mafunzo ya uwalimu.


Kauli hiyo imetolewa na kwa nyakati tofauti na Afisa Mfawidhi wa mfuko huo mkoa wa Mara,Sudi Hamza alipokuwa akizungumza na wanachuo hao katika semina zinazoendelea kutolewa na mfuko huo katika kuwaandaa walimu hao mfuko sahihi wa kujiunga na kupata pensheni mbalimbali kwa wakati.


Amesema wakati wanachuo hao wakiwa bado hawajapata ajira wanaweza kujiunga na uchangiaji wa hiari ambapo pia unapata mafao kutokana na mpango huo na kumuomba kila mmoja kuchngamkia fursa ya kujiunga na mpango huo.


Sudi amesema kiwango cha uchangiaji ni kuanzia kiasi cha shilingi 10,000/= au zaidi na michango inaweza kuwasilishwa kwa njia rahisi ya simu ya mkononi kupitia M-Pesa,Tigo-Pesa,Aitel Money na wakala wa Max Malipo huku wanachama wakiwa huru kuwasilisha michango yao kwa wiki,mwezi au msimu.


Amesema mchangiaji wa hiari anapata Fao la Ujasiliamali kuongeza mtaji na kuanzisha biashara,Fao la Uzeeni,Fao la Kifo,Fao la Elimu,ambalo litamfanya mchangiaji kwenda kuongeza elimu yake,Fao la Ugonjwa na Ulemavu,Fao la Matibabu pamoja na Fao la Kujitoa.


Afisa huyo wa PSPF mkoa wa Mara amesema kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari imeanzisha fao la matibabu kwaajili ya wanachama wake walioko katika sekta isiyo rasmi ambapo mpango huo ni ushirikiano kati ya PSPF na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF).


Wanachuo katika vyuo hivyo wameupokea  mpango huo na kuamua kujiunga kwa wingi kwa kujaza fomu za uchangiaji wa hiari ili kujiwekea mazingira mazuri ya kupata mafao ambayo yatawasaidia katika maisha yao.

 Wanachuo wa chuo cha ualimu cha Musoma Utalii wakifatilia kipeperushi cha PSPF wakati wa semina chuoni hapo
 Ufatiliaji ukiendelea
 Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Mara,Sudi Hamza,akizungumza na wanachuo wa Musoma Utalii

 MR.Daudi kutoka PSPF akiendelea kutoa somo kwenye semina chuo cha Musoma Utalii
 Moja ya wanachuo akifatilia kipeperushi kwa makini
 Msisitizo ukiendelea
 Ni kama anasema "jamani mmeelewa"

 Miss.Robby kutoka PSPF mkoa wa Mara akiendelea kugawa fomu kwaajili ya kujiunga na uchangiaji wa hiari katika Chuo cha Musoma Utalii
 Moja ya wanachuo akiuuliza swali
 Sudi akiendelea kutoa ufafanuzi

 Sudi akiwa na washindi waliojibu maswali yaliyoulizwa kuhusu ufahamu na  PSPF ambao walipata zawadi
 Zawadi za fedha taslim zikitolewa


 Hapa elimu iliamia chuo cha Mtakatifu Alberto
 Wana chuo wa Mtakatifu Alberto wakijaza fomu za kujiunga na mfuko wa uchangiaji wa Hiari
 Daudi akitoan zawadi kwa washindi wa kujibu maswali katika chuo cha Mtakatifu Alberto
 Zawadi zinaendelea kutolewa

Post a Comment