2

 
 MKURUGENZI wa The Grand Victoria Hotel ya mjini Musoma,Ramadhani Msomi Bwana,amechangia fedha taslim shilingi milioni 3 kwaajili ya utengenezaji wa madawati kwenye shule aliyosoma ya Kinesi iliyopo wilayani Rorya mkoa wa Mara na kuahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 150 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule zote za Tarafa ya Suba wilayani hapo.

Msomi ameyasema hayo mara baada ya kumkabidhi Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara,Christopher Sanya, kama mmoja wa wananchi wa Tarafa ya Suba kwaajili ya kukabidhi kwa viongozi wa serikali wakiwemo madiwani wanaotoka kwenye maeneo hayo.

Amesema anajua umuhimu wa elimu na changamoto zilizopo katika kufikia elimu bora hivyo kutokana na kipato alichokipata kutokana na shughuli zake ameamua kutoa kiasi hicho cha fedha ili kuweza kusaidiana na serikali na wadau wengine katika kuinua elimu na kufikia malengo ya elimu bora kwa kila mmoja
Sehemu ya vifaa vya wanafunzi alivyovitoa
Rama Msomi Bwana(kushoto)akiangalia moja ya jengo la darasa la shule ya Kinesi A lililochakaa

 Rama akikabidhi vifaa na fedha kwa walimu wa shule ya msingi Kinesi A
 Moja ya vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwa nguvu ya Rama Msomi

 Wanafunzi wa shule ya msingi Kinesi A wakiwa wamekaa kwenye mawe wengine chini ambapo Rama Msomi,aliamua kuchangia kutengeneza madawati
 Adha ya kupata elimu darasani
 Rama akiwa na viongozi wa Tarafa ya Suba
Milioni 3 za kuanzia zilizotolewa na Ramadhani Msomi Bwana


Post a Comment