KUANZA kwa Chuo Kikuu cha Kilimo na Sayansi cha
Mwalimu Julius K.Nyerere,kilichopo wilayani Butiama mkoa wa Mara kitaupandisha
na kuuinua mkoa katika masuala mbalimbali pamoja na kuwasaidia wakulima katika
kuinua kilimo.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa
Mara,Magesa Mulongo,alipotembelea sehemu ya majengo ya iliyokuwa shule ya
Osward Mang'ombe High School ambayo yatatumika kama "campas"ya chuo
hicho kinachotarajiwa kuanza kupokea wanafunzi oktoba mwaka.
Amesema chuo hicho ambacho kitatoa shahada na stashahada
za fani mbalimbali licha ya masuala ya kilimo itakuwa chachu kubwa ya maendeleo
ya mkoa wa Mara na wananchi watakaokuwa wanazunguka mazingira ya chuo na
kuwataka wananchi kujiandaa kukipokea.
Mulongo ambaye alikuwa ameongozana na viongozi wa
ngazi ya wilaya,alisema cha kwanza ambacho kinapaswa kuangaliwa ni kuhakikisha
migogoro ya aina yoyote baina ya chuo na wananchi haipatikani yakiwemo masuala
ya ardhi ili uongozi wa chuo ufanye
shughuli zake bila kubugudhiwa.
"Kwanza ni heshima kubwa kuwepo na kuletwa
kwa chuo hiki mkoa wa Mara na hususani kwenye wilaya ya Butiama katika kumuenzi
mzee wetu Mwalimu Julius Nyerere na ni muhimu kinapokwenda kuanza kusiwepo na
vikwazo vya aina yoyote.
"Lakini chuo hiki kitaupandisha na kuuinua
mkoa wa Mara maana mahala popote palipo na vyuo au chuo kikuu licha ya mkoa
kunufika lakini pia wananchi wananufaika kutokana na fursa mbalimbali ambazo
watazipata kutoka kwa wanachuo,"amesema Mulongo.
Amesema kutokana na taarifa ambazo amepewa na
uongozi wa chuo hicho,wananchi wakulima wa kawaida pia watapata fursa ya kupata
kozi fupi ambazo zitawasaidia kuboresha shughuli zao za kilimo na kuwaomba
wananchi kujiandaa na hilo.
Akitoa taarifa ya chuo hicho baada ya kuteuliwa
na Rais wa awamu ya nne,Jakaya Mrisho Kikwete,kuanza mchakatato wa chuo
hicho,Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaruma,profesa Lesakit Mellau,amesema
wameshafikia hatua kubwa ya kuanza kwa chuo hicho ikiwemo kuanza kuajili
wahadhiri.
Amesema bado kuna masuala ya fedha kutoka
serikalini yasubiliwa kutokananza kupokea na bajeti na mambo yakienda vizuri
kufikia oktoba wataanza kupokea wanafunzi.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Butiama
waliozungumza na Mtanzania kuhusiana na chuo hicho walisema wapo tayari kutoa
ushirikiano kutokana na manufaa ambayo watayapata kutokana na kuwepo kwa chuo
hicho katika maeneo yao.
Mulongo alipokuwa akiingia maeneo ya chuo hichoAkianza mazungumzo
Sehemu ya majengo ya chuo |
Masomo yataanzia hapa
Post a Comment
0 comments