0
CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU MKOA WA MARA – FAM
Affiliated to TFF
YAH: MAAMUZI YA TFF, KAMPENI ZA WAGOMBEA  NA UCHAGUZI.
Leo tarehe 14/6/2016, Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha  Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) kwa mujibu wa Katiba ya FAM, Kanuni za uchaguzi TFF  na baada ya kupokea maamuzi  ya malalamiko toka TFF, katika barua ya tarehe 13/6/2016 yenye kumbukumbu namba TFF/ADM/LM.39/2016 inapenda  kuwatangazia  wanachama wa FAM, wadau wa michezo na umma kwa ujumla kupitia magazeti, radio, TV na mbao za matangazo kuwa wagombea wafuatao wamekidhi vigezo  kwa mujibu wa katiba ya FAM na Kanuni za uchaguzi za TFF na wanapewa nafasi ya kugombea nafasi kama walivyoomba; wagombea hao ni;
 1. MICHAEL Richard Wambura              Nafasi ya mwenyekiti.
 2. MAGATI Zamberi  Francis                     Nafasi ya  makamu mwenyekiti.
 3. SAMWELI Silas                                         Nafasi ya  katibu.
 4. REVOCATUS Mashauri Kuboja            Nafasi ya Katibu.
 5. BENARD S. Sakira                                  Nafasi ya katibu.
 6. EJAGA  Mahamba                                   Nafasi ya mweka hazina.
 7. MOSES Timoth Kimwaga                     Nafasi ya mweka hazina
 8. MUGISHA M. Galibona                          Nafasi ya mjumbe  mkutano mkuu.
 9. MUGETA Mtete                                        Nafasi ya mjumbe mkutano mkuu
 10. YAMO Odemba Kagose                          Nafasi ya mjumbe mkutano mkuu
 11. ELIUD William Bwire                          Nafasi ya mwakilishi wa vilabu.
 12. KILIGINI Mabalaja Bandoma             Nafasi ya mwakilishi wa  vilabu.
 13. GORDON P.M. Mumbara.                    Nafasi ya mwakilishi wa vilabu.
Wagombea tajwa hapo juu wanaruhusiwa kuanza kampeni kama inavyoonyesha katika ratiba iliyotolewa tarehe 11/4/2016, na kwamba uchaguzi ni tarehe 18/6/2016.
Pia TFF imemwengua  mgombea ndugu Sospiter Masambu Aliyekuwa anagombea nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu TFF kwa kosa la kukiuka katiba ya FAM ibara ya 7 Kifungu cha 2(d).
Nawatakieni  wagombea wote kampeni njema zenye kufuata maadili kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
“MICHEZO NI FURAHA, AFYA NA AJIRA”
WAKILI OSTACK MLIGO
MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI FAM

Post a Comment