0

MWENYEKITI wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Mara (FAM),Michael Richard Wambura, ameanza mikakati ya kuinua soka la mkoa wa Mara siku 2 baada ya kuchaguliwa nafasi hiyo ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfuko wa maendeleo ujulikanao kama Mara Football Deveropment Fund (MFDF).

 Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kufanyika kwa kikao cha cha kwanza cha kamati yautendaji akiwa Mwenyekiti wa kikao hicho,Wambura amesema wana Mara wawe na mshikamano na kuamini kuwa mabadiliko na maendeleo ya kweli yanakuja ikiwemo kuona ligi kuu msimu ujao.
 Tayari mkuu wa Mkoa wa Mara,Magesa Mulongo,amekubali kuwa mlezi wa mfuko huo utakaoanzishwa rasmi siku chache zijazo baada ya kukutana na Mwenyekiti huyo ofisini kwake na kuonyesha mwanzo mzuri wa ahadi za Wambura.Post a Comment