0
 CHAMA cha mpira wa Miguu mkoa wa Mara(FAM),kimeanza kutekeleza mpango wake wa kuandaa makocha na waamuzi wa mchezo huo ili kupata wataalamu wa kutosha ambao wataweza kufundisha na kutoa maamuzi uwanjani.

Mpango huo umeanza kwa kufundishwa waamuzi wa soka ngazi ya awali kama alivyotoa ahadi Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mara,Michael Wambura,mara baada ya kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo miezi michache iliyopita.

Akifungua mafunzo hayo kwa waamuzi wapya wapatao 23 wakiwemo watoto 2 waliomaliza elimu ya msingi mwaka huu,Afisa Michezo wa mkoa wa Mara,Evance Sangawe,amesema chama cha soka kimeanza kutekeleza mpango mzuri kwa kuwa bila waamuzi hakuna mchezo utakaoweza kuchezeka.

Amesema mpango huo utaweza kuzalisha waamuzi wengi kwenye wilaya mbalimbali za mkoa kwa kuwa waamuzi hao wametoka kwenye maeneo ya wilayani ambapo kumekuwa na uhaba mkubwa wa waamuzi.

Sangawe amesema kutokana na kukosekana kwa waamuzi wa kutosha kulipelekea kuibua migogoro ambayo inahusiana na maamuzi na kuwaomba wanaosomea fani hiyo kuzingatia mafunzo yote watakayofundishwa.

Mkufunzi wa waamuzi ambaye pia ni kamishina wa FIFA wa kusimamia michezo,Alfred Lwiza,amesema sheria za mpira zimebadilika hivyo waamuzi wapya na wazamani wanatakiwa kuzisoma na kuzifatilia sheria hizo ili waweze kuzisimamia vizuri uwanjani.

Amesema sheria namba 12 ya mchezo imebadilika ambapo kosa linaweza kuchezwa nje ya uwanja na kisha adhabu ikaja kuchezwa uwanjani hivyo kila mmoja wakiwemo waamuzi na makocha ni muhimu kufahamu na kushukuru (FAM) kwa kuandaa mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo walitoa pongezi upatikana kwa mafunzo hayo na kudai kutokana na kuupenda mchezo huo wamekuwa wakichezesha michezo mbalimbali bila kuzijua sheria na kudai baada ya mafunzo hayo na menine watakayoyapata kutawafanya kuwa waamuzi bora.

 Elimu ikiendelea darasani








 Baadhi ya waamuzi watarajiwa wakizungumzia elimu wanyoipata

Post a Comment