0

"Tumeendelea na kampeni ya kutokomeza BANGI wilayani Tarime. Bangi ilifika wakati inalimwa waziwazi kama vile ni zao halali jitihada hizi za kufyeka na kuchoma zinapeleka ujumbe haraka kwa jamii kuwa zao hili ni haramu na haliruhusiwi. Tumeteketeza kwa kufyeka hekari 30 pia tumekamata mbegu kilo 50 na kubaini mashamba mapya yaliyopandwa zaidi ya 15 tutarudi kufyeka itakapomea. Natoa wito kwa wananchi kuachana na kilimo cha Bangi kwani hairuhusiwi kisheria na tutahakikisha inaharibiwa kabla hawajavuna. Ardhi ya Tarime itumike kulima mazao halali tu"kauli ya mkuu wa wilaya ya Tarime,Gluorius Luoga,alipokuwa anaendelea na oparesheni tokomeza bangi.

 Bangi ambayo tayari ilikamatwa ikiwa ndani ya mifuko
 Maelekezo yakitolewa na mkuu wa wilaya
Sehemu ya shamba moja la bangi

 Mkulima akiwa na junia la bangi

 Mkuu wa wilaya akimuelekeza mkulima pa kwenda
 Hapa ilikuwa mwendo wa kwenda kwenye mashamba
 Kikosi kazi cha kuteketeza mashamba ya bangi


Haikuwa kazi ndogo

 Jamaa wengine walifunikia bangi bendelea ya chama cha siasa

Post a Comment