0
HATIMAYE UPUNGUFU MKUBWA WA MADAWATI KATIKA SHULE ZA MSINGI AMBAO BADO ULIKUWA UKIIKABILI WILAYA YA RORYA MKOANI MARA UMEPATIWA UFUMBUZI BAADA YA KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA TIGO KUTOA MSAADA WA MADAWATI 235 YENYE THAMANI ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 39 AMBAYO YATASAMBAZWA KATIKA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI WILAYANI HUMO.

AKIZUNGUMZA WAKATI WA HAFLA YA KUKABIDHI MA  WADATI HAYO KATIKA SHULE YA MSINGI UTEGI WILAYANI RORYA,AMBAYO PIA YATASAMBAZWA KWA SHULE 17 ZA MSINGI MKOANI MARA,MENEJA WA TIGO KANDA YA ZIWA BW EDGA MAPANDE,AMESEMA KAMPUNI HIYO IMETOA MADAWATI HAYO KATIKA KUUNGA MKONO JUHUDI  ZA SERIKALI YA AWAMU YA TANO  KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO YA MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI NCHINI

NAYE MKUU WA MKOA WA MARA DK CHARLES MLINGWA,AKIZUNGUMZA BAADA YA KUPOKEA MADAWATI HAYO,AMEIPONGEZA KAMPUNI HIYO YA SIMU ZA MKONONI YA TIGO KWA KUUNGA MKONO JUHUDI HIZO ZA SERIKALI KATIKA KUTATUA CHANGAMO ZINAZOIKABILI SEKTA YA ELIMU MKOANI MARA


TAYARI KAMPUNI HIYO SIMU YA TIGO IMETOA MADAWATI 1,275 YENYE THAANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 211 KWA SHULE ZA MSINGI KWA MIKOA YOTE YA KANDA YA ZIWA.
EDGER(KULIA) AKIMKABIDHI MADAWATI MKUU WA MKOA


Post a Comment