0


TIMU za Polisi Mara Veterani na Biashara United za mjini Musoma,leo zitacheza mchezo maalum katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume mjini Musoma ikiwa ni moja ya mchezo wa kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza na Blog hii,Mwenyekiti wa timu ya Biashara United,Selemani Mataso,amesema Mwalimu Nyerere alikuwa ni kiongozi mwanamichezo hivyo kwa kutambua umuhimu wake wameamua pia kushirikiana na timu ya Polisi veterani kumuenzi.

Amesema Mwalimu Nyerere alikuwa ni mshiriki mkubwa wa michezo mbalimbali aliyokuwa akishiriki yeye mwenyewe na mingine akiishuhudia na kudai kila mmoja anapokuwa katika kumbukumbu yake ni vyema akafanya kitu cha kimichezo katika kumuenzi.

Mataso amesema ili kumuenzi ipasavyo kupitia sekta ya michezo ni wanamichezo wote kuhakikisha wanadumisha upendo michezoni na ndio itakuwa njia sahihi ya kumuenzi.

Mwenyekiti huyo ambaye amekuwa akifanya jitihada za kuhamasisha watu mbalimbali kushiriki michezo hususani watu wenye umri mkubwa na wachezaji wa zamani alidai mchezo huo utakuwa chachu zaidi ya kuhamasisha michezo.

Nahodha wa timu ya Polisi veterani,Godfrey Rwegasira,amesema licha ya timu ya Biashara United kufanya mazoezi kwa muda mrefu lakini watahakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo huo wa kumuenzi Mwalimu Nyerere.

Amesema wanao wachezaji wazuri ambao wanaamini watafanya vizuri kwenye mchezo huo ambao pia unatarajiwa kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa michezo mjini Musoma.

Aidha timu nyingine kutoka taasisi mbalimbali zinatarajiwa kushiriki katika kumbukumbu hii ya mwalimu

Post a Comment