0

   MKUU wa Wilaya ya Tarime,Glorius Luoga,amesema taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti moja la kila siku linalochapishwa hapa nchini kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara,Christopher Sanya, alitoa Rushwa kwenye kikao cha halimashauri kuu ya CCM kwaajili ya kupokea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho sio za kweli na zilipikwa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake,Luoga amesema kikao hicho kilikuwa ni chake kwaajili ya kutoa taarifa ya utekelezaji wa ilani na alikigharamia yeye kupitia pia michango ya wadau wa chama hicho na hakuna fedha yoyote iliyotolewa na Mwenyekiti huyo kama ilivyoandikwa.


 Amesema chakula kilichokuwa kimeandaliwa na kiasi cha shilingi 15000 kwaajili ya nauli kwa wajumbe kuwarudisha majumbani yeye ndio aliyoitoa kwa kumkabidhi katibu wa chama wa wilaya na kupewa risti  chama na kuomba unapoelekea wakati wa uchaguzi wanachama wa CCM wasianze kutafuta taarifa za kuchafuana.

"Nimeamua nitolee taarifa haya yaliyoandikwa kwenye gazeti hili kwa kuwa ni taarifa za uongo na ambazo hazipaswi kufumbiwa macho na mimi mwenye kikao kile nikakaa kimya bila kutoa ufafanuzi.
 "Fedha zile nilizitoa mimi ambapo pia zilichangiwa na marafiki wa chama wajumbe wakapata chakula na nauli za kuwarudisha majumbani Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mara ambaye pia alihudhuria kikao hicho hakutoa kiasi chochote cha fedha,"alisema Luoga.Post a Comment