0

KLABU ya michezo ya Biashara United, yenye maskani yake mjini Musoma,imefanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya watakaoingoza kwa kipindi cha miaka 2 huku uchaguzi huo ukifanyika kwa amani na utulivu wa hali ya juu.
 
    

















 Uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Musoma Club ulimrudisha madarakani Mwenyekiti wa kwanza wa club hiyo,Selemani Mataso na Katibu aliyekuwa pia kwenye uongozi uliopita,Yuhana Mtambalike.

Viongozi wengine waliochaguliwa na nafasi zao kwenye mabano ni,Christiana Samo(Makamu Mwenyekiti),Elias Katogoro(Katibu Msaidizi),Ghat Marwa(Mweka Hazina),Marwa William)Meneja wa timu) huku wajumbe wa kamati ya utendaji waliochaguliwa ni,Shomari Binda,Augustine Mgendi,Melvin Nashon,Noar pamoja na Frenk Wabare.


 Akizungumza mara baada ya kutangazwa kwa matokeo na Mwenyekiti wa uchaguzi huo,Said Gantala,Mwenyekiti mteule wa club hiyo,Selemani Mataso,aliwaomba viongozi wote waliochaguliwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kushirikiana ili kuweza kusukuma mbele maendeleo ya timu hiyo.
 

Alisema uongozi wa timu hiyo ni uongozi wa kujitoa hivyo ni vyema kila kiongozi aliyechaguliwa kuona jukumu la kuiongoza timu hiyo ni lake na asiachiwe mtu mmoja kufanya kila jambo kwani kufanya hivyom kutaifanya club hiyo kutokusonga mbele.

 Mataso alisema club ya Biashara United imeanza kuwa kubwa kwani ilianzishwa kama sehemu ya kukutana wachezaji wa zamani lakini kwa sasa inakwenda kuwa na timu za vijana na kuziingiza kwenye ligi huku wakongwe wakiendelea kuwa na timu yao hivyo ni muhimu kuwa na viongozi wanaojituma.
 

"Tumemaliza uchaguzi wa kuwapata viongozi kwa amani nakila mmoja amefurahi,sasa kilichobaki ni kufanya kazi kwa kushirikiana ili yale ambayo tumekusudia kuyafanya kwenye timu yetu yaweze kufanikiwa,"alisema Mataso.
 Mjumbe wa Mkutano mkuu wa uchaguzi wa timu ya Biashara United,Frola Yongolo,akichangia jambo kwenye mkutano huo
 Wajumbe wakifatilia mkutano

 Mwenyekiti wa uchaguzi,Said Gantala,"Jecha"akionyesha kura iliyopigwa
 Mijadala ikiendelea
 Kura zikihesabiwa na wasimamizi wakiongozwa na "Jecha"
 Uchaguzi ulikuwa si mchezo
 Chini viongozi waliochaguliwa chini ya Mwenyekiti,Selemani Mataso

Post a Comment