Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua kikao cha wadau wa Mfuko wa Bima ya Afya mkoa wa Mara(NHIF) kilichofanyika kwenye ukumbi wa uwekezaji wa mkoa na kusema kwa sasa kila mmoja anapaswa kubadilika na kuzingatia taratibu zote za utoaji wa huduma za afya katika sehemu yake ya kazi.
Katika kikao hicho ambacho kimehudhuliwa pia na Bodi ya mfuko huo chini ya Mwenyekiti wake Anne Makinda na wajumbe wake,amesema tabia mbaya ambazo zinafanywa na wataalam hao wa afya za kuwanyanyapaa wanaotumia mfumo wa kadi hazikubaliki na lazima zikome kwa kila mmoja.
Amesema zipo taarifa ambazo zinawahusu wauguzi na madaktari ambao wanafanya tabia hizo na kwa sasa yeye akiwa kama kiongozi wa mkoa hawezi kukubali jambo hilo lifanyike na atakaye jaribu kufanya hivyo atafukuzwa kazi.
Mlingwa amesema serikali ina mpango wa kuhakikisha kila mtanzania anaingia kwenye mfumo wa kupata huduma ya afya kwa kutumia mfumo wa kadi na wale wanaokwamisha huduma kwa sasa kwa wanaotumia kadi ni vyema wakachukuliwa hatua.
Mkuu huyo wa mkoa amesema mikakati ya mkoa kwa sasa ni pamoja na kuongeza kaya zinazotumia kadi za CHF na ambayo mfuko inataraji kuboresha zaidi ili kuweza kuwa na wanachama wengi kwenye wilaya zote za mkoa wa Mara.
Akizungumza kwenye kikao hicho,Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF),Anne Makinda,amesema vituo vya afya vya serikali ndivyo ambavyo vinaongoza kwa wahudumu wake kutoa huduma zisizofaa kwa wateja wanaotumia mfumo wa kadi na kuwataka kubadilika kwa kuwa wanapoteza hadhi ya vituo.
Amesema NHIF inazihudumia na kutoa vifaa tiba,madawa na mbalimbali kwenye vituo vya afya kwa mujibu wa taratibu lakini bado kumekuwa na malalamiko ya wateja wanapokwenda kutibiwa kukutana na vikwazo na kupelekea kuonekana wamepotea njia kutumia mfumo wa bima ya afya.
Makinda amesema inapaswa kuzingatia hupatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika zahanati,vituo vya afya na hospitali inakuwa sio tatizo ili kila mmoja anayekuwa anatumia kadi kwaajili ya kupata huduma ya afya asiweze kupata tabu na kuangaika.
Akitoa taarifa ya kitaifa ya mfuko huo,Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Bernard Konga,amesema mfuko huo unatoa huduma zote kwenye vituo 6998 ambavyo vimesajiliwa kutoa huduma na mfuko ambapo vingi ni vya serikali na kutoa wito wa kutoa huduma bora kwenye vituo hivyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF)Bernard Konga,akitoa taarifa ya kitaifa ya mfuko huo kwenye kikao cha wadau wa mkoa wa Mara
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Mara,Latens Wella.akitoa taarifa ya mkoa kwenye mkutano wa wadau
Afisa uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Mr Singu,(kulia)akifatilia kikao hicho(kushoto ni afisa wa mfuko huo mkoa wa Mara,Athumani Said wakifatilia kikao hicho
Wadau wakifatilia na kuchangia kwenye kikao hicho
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya,Tryphon Rutazamba,akizungumza kwenye kikao hicho ambapo aliusifu mji wa Musoma kwa usafi wa mji na kufanya kikao chenye majadiliano mazuri
Wadau wakifatilia
Post a Comment
0 comments