0


OPARESHENI ya siku 2 iliyoongozwa na mkuu wa wilaya ya Tarime,Glorius Luoga,Kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime/Rorya,Andrew Satta pamoja na vikosi vya mbalimbali vya ulinzi na usalama imefanikiwa kufyeka mashamba 37 ya bangi wilayani humo.
Licha ya mashamba hayo yenye ukubwa wa ekali 56 pia walifanikiwa kukamata magunia 20 ya bangi kavu yenye uzito wa tani 1 ambayo ilikuwa imeshaandaliwa na kutunzwa kwaaajili ya kupelekwa sokoni.
Akizungumzia oparesheni hiyo iliyofanyika Kijiji cha Nyarwana na Matongo Kata ya Kibasuka,ambayo pia iliwashirikisha wananchi katika kufysheka mashamba hayo,mkuu wa wilaya ya Tarime,Glorius Luoga,amesema katika oparesheni zote ambazo wamekuwa wakizifanya  hii imefanikiwa zaidi.
Amesema kiasi kikubwa cha mashamba na magunia ya bangi ambayo yamekamatwa imetokana pia na ushirikiano ambao waliupata kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo.
Luoga amesema mikakati kabambe inaendelea kuandaliwa katika kukomesha kilimo cha bangi ikiwemo kuanzisha kilimo cha miwa katika mabonde ambayo kunafanyika kilimo cha bangi na hatua mbalimbali zinaendelea katika kulifamnikisha hilo.
"Tulianza mapema kupambana na zao haramu la bangi na maagizo kutoka ngazi ya ntaifa itaendelea kutusukuma zaidi katika mapambano haya na naamini tutafanikiwa na hizi oparesheni tunazoendelea nazo zinatusidia.
"Kuna watu ambao kuna jitihada ambazo tunazifanya katika kukomesha kilimo cha bangi kwa kuongea na wawekezaji kwaajili ya shughuli nyingine za kilimo wanakuwa kama wanakwamisha sasa hatuwezi kukubaliana nao na tutawashughulikia,"amesema Luoga.
Amesema muda umefika kwa wale wanaojihusisha na kilimo cha bangi kujisalimisha na kuachana na zao hilo haramu na kudai muda utakapofika watatangaza rasmi mpango kabambe wa kilimo cha miwa wilayani Tarime ambacho kitawasukuma kuachana na kilimo cha bangi.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya,Andrew Satta,amesema katika oparesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 14 ambao wanajishughulisha na kilimo cha bangi ambao bado wanaendelea kuwahoji na upelelezi utakapokamilika watafikishwa Mahakamani



DC luoga akifyeka mashamba ya bangi
Polisi wakimuhoji mmoja wa watu waliokamatwa wakidaiwa kujihusisha na kilimo cha bangi
 
DC akiluka viunzi kufuata mashamba ya bangi


 kazi shirikishi katika kupambana
 Ni mwendo wa kufyeka bangi

 JWTZ piua walikuwepo na vikosi vingine katika oparesheni
 Bangi
 Mbegu za bangi pia zilikamatwa
 Watuhumiwa wakishusha bangi iliyokamatwa

 Oparesheni ilikuwa kali
 Chini Waandishi wakila viazi vya kuchoma kwenye oparesheni hiyo

Post a Comment