0

 
 VIJANA wanaocheza mpira wa miguu katika manispaa ya Musoma,wamewapongeza wawekezaji kutoka Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) kuhamasisha michezo mara kwa mara kwa kuandaa mashindano.

Wakizungumza na BLOG hii mara baada ya mchezo wa fainali wa mashindano ya Sura Cup,vijana hao wamesema kufanyika kwa mashindano mara kwa mara kunachangia kuhamasisha mchezo wa soka na kuwafanya kucheza mpira kwa muda mrefu.


Nahodha wa timu ya Baruti Fc, walioibuka mabingwa wa mashindano hayo kwa kuifunga timu ya MeTL fc Mabao 4-3,Rashid Juma,amesema hamasa ambayo imekuwa ikifanywa na kampuni hiyo kwa kuandaa mashindano ya vijana inapaswa kuungwa mkono na wadau wengine wakiwemo viongozi wa mpira
amesema mashindano ambayo yamekuwa yakiangaliwa yamekuwa yakiwaleta vijana pamoja na wapo waliotokea kwenye michezo inayokua inaandaliwa wanacheza kwenye timu mbalimbali mkoani Mara.

Rashidi alisema baada ya kumalizika kwa ligi ya wilaya pamoja na ligi ya mkoa kwa msimu wa mwaka 2015-2016 sasa wadau wanapaswa kuelekeza nguvu kwenye mashindano mengine ili vijana waendelee kucheza mpira.

Kocha wa timu ya Baruti Fc,Abdara Musa,ambaye baada ya timu yake kuwa mabingwa walikabidhiwa kikombe na fedha taslimu shilingi 150,000,alisema mashindano hayo ni njia ya kuinua vipaji vya vijana na kuipongeza kampuni hiyo kwa kubuni mashindano mara kwa mara.

Meneja masoko wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL),tawi la Musoma,Kalpesh Limbachy(anyekabidhi kombe hapo chini),amesema kufanya mashindano ya mara kwa mara ni kurudisha shukrani kwa wateja wao na mashindano hayo ni mwendelezo wa mashindano mbalimbali.
 

Amesema kwa kutambua umuhimu wa michezo hususani kwa vijana wataendelea kuandaa mashindano na kuboresha zaidi zawadi ili kuwavutia vijana wengi kuweza kushiriki.

Post a Comment