0

UONGOZI na wafanyakazi wa kampuni ya New Space 2000 inayojishughulisha na shughuli za burubudani kwenye mji wa Musoma hususani kwenye ukumbi maarufu wa Disco wa The Club House zamani ukiitwa Metropole,leo wametoa misaada mbalimbali ya dawa,Gloves pamoja na sabuni kwenye kituo cha afya Nyasho pamoja na hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara ambapo mmoja wa Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Abubakar Nyamakato"Dj Abuu"amesema msaada huo umetokana na kipato kidogo kinachopatikana kutokana na shughuli wanazozifanya.
 Abuu akizungumza na uongozi wa kituo cha afya Nyasho kabla ya kukabidhi misaada waliyopeleka
 Meneja Hassan"Mwili Nyumba"akiwa na Chacha wakifatilia kwa karibu
 Mkurugenzi Abdara Malima,akizungumza kile walichokipeleka kwenye kituo cha afya Nyasho
 Wafanyakazi wakipeleka sabuni kwenye wodi za wagonjwa
 Misaada ikiendelea kutolewa

 Uongozi wa New Space wakikabidhi msaada kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyasho,Michael Mwita
 Wafanyakazi wa New Space wakifurahia jambo
 Misaada ikitolewa wodini


 Shukrani ikitolewa baada ya kukabidhi misaada

 Hapa ni kwenye hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara,wafanyakazi wa New Space wakizungumza na Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospital hiyo,Dk.Bisanda Hosea baada ya kufika kwenye hospital hiyo kwaajili ya kukabidhi misaada yao 
 Ni utulivu katika kumsikiliza Dk.Bisanda

 Dk.Bisanda akisisitiza jambo
 Dj Timba na Mkurugenzi Abdara Malima wakisikiliza kwa makini
 Chini msaada ukikabidhiwa kwa Dk.Bisanda

Post a Comment